Saturday, June 20, 2009

E-Club

E-Club ni nini?

Usikose hapa hapa sayuni..inakuja kuleta mapinduzi ya kifikra mapema iwezekanavyo

Thursday, June 11, 2009

Kongamano la Wajasiliamali lafana sana

Kongoma kubwa la wajasiliamali lililoandaliwa na kampuni inayokua kwa kasi sana hapa nchini ya DigitalBrain lilifana sana siku ya jumamosi tarehe 6/6/2009.


Katika kongomano hilo ambalo wajasiliamali takribani ya 120 walihudhuria na kupewa mafunzo ya kina kabisa jinsi ya kufanikiwa kibiashara na kubadirishwa mtazamo wao kutoka ule wa "utumwa" wa kuajiriwa na kuwa na ule wa "kifalme" wa kujiajiri na kumiliki biashara.
Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa Mbinga mashariki -CCM Mheshimiwa Gaudency Kayombo, alisema kuwa amefurahishwa sana na hatua iliyochukuliwa na DigitalBrain ya kuwaleta wajasiliamali kwa pamoja na kuwafundisha masomo hayo ambayo yanalenga katika kuwakomboa watanzania na wimbi la umaskini.


Walimu mbalimbali walifundisha masomo yapatayo 8 na kuwafanya wahudhuriaji kutaka DigitalBrain waandae kongomano jingine kama hilo mapema iwezekanavyo.



Wahudhuriaji wengi walitoka hapa Dar,Kibaha,Arusha,DRC-Congo na hata Ufaransa.



Habari zaidi zitafuata hapo baadaye.