Monday, January 25, 2010

Kakobe Vs Tanesco

ASKOFU mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zacharia Kakobe ameligomea Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitisha mbele ya kanisa lake njia ya umeme ya msongo mkubwa wa kilovolti 132.Akofu huyo pamoja na mamia ya waumini wake, jana walikusanyika mbele ya kanisa hilo lililo kando ya Barabara ya Sam Nujoma karibu na Mwenge, jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kupambana baada ya kupata taarifa kwamba mafundi wa Tanesco wangewasili kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kupitisha njia hiyo ya umeme.
"Mimi nimejiandaa kuongoza waumini wangu katika kukabiliana na yeyote. Mimi nipo tayari kufa na nitahakikisha hawapitishi njia hiyo labda wawe wameniua," alilalamika.Alilalamika kuwa iwapo umeme wa msongo huo utapitishwa eneo hilo utaathiri mitambo inayosaidia kunasa, kupaza na kurekodi sauti kwenye ibada zinazofanyika kanisani hapo pamoja na mpango wake wa kuanzisha kituo cha televisheni cha kanisa.
Isitoshe, alisema kwamba tayari Tanesco wamemuarifu kuwa itabidi wayang'oe mabango mawili ambayo yaligharimu Sh120 milioni ili kupisha mradi huo."Kama Watanzania haijatokea vita ya dini, basi ndiyo hii. Ni kubwa kuliko ile ya Wabarbeig," alisema Askofu Kakobe na kuitaka serikali iingilie kati suala hilo ili kuepusha dhahama inayoweza kutokea."Mimi na waumini wangu tumekubaliana tutakesha hapa usiku na mchana. Maana nasikia huwa wanaweza kuja usiku kubomoa mabango haya," alisema Askofu huyo mwenye maelfu ya waumini jijini Dar es Salaam.Mwananchi lilipowasili jana eneo hilo ilikuta mamia ya waumini hao pamoja na Askofu Kakobe wakionekana kutokuwa na silaha yoyote lakini wakisisitiza kuwa wako tayari kwa vita dhidi ya mtu yeyote atakayefika eneo hilo kwa lengo la kung'oa mabango yao."Walifikiri kwa kuwa sisi ni walokole tutakaa kimya, lakini sisi tunasema katika hili hakuna cha kusema tutamwachia Mungu. Mungu yuko 'busy' (anakabiliwa na majukumu mengi) ana kazi nyingi, hili ni jukumu letu," alisema Askofu Kakobe.Alilalamika kwamba utawala wa Rais Kikwete unalikandamiza kanisa lake huku akidai kuwa kama ingekuwa madhehebu mengine ya dini, kitendo kama hicho kisingetokea."Wanachokifanya hakina adabu! Kwa (askofu mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp) Pengo isingekuwa rahisi.
Wanamuonea Kakobe kwa kuwa ni mnyonge," alilalamika Kakobe akisema yuko tayari kufa ili mradi ahakikishe njia hiyo ya umeme haiwekwi karibu na kanisa lake.Alibainisha kuwa awali njia hiyo ilikuwa ipite upande wa pili wa barabara mkabala na kanisa hilo, lakini wakazi wengi wa eneo hilo walipinga kitendo hicho hata pale walipoahidiwa kufidiwa."Hawa waliokataa, hata pale walipoahidiwa kufidiwa, wengi ni wasomi wa chuo kikuu. Eneo hilo ndilo lenye nafasi kubwa. Lakini wakaona upande huu hauna wasomi wanaweza kukubali kirahisirahisi tu.Mimi katika hili nasema hapana," alisema Kakobe.Kakobe alisisitiza kuwa yeye na waumini wake wameamua kuwa watakuwa wakikesha eneo hilo kuhakikisha watapambana na yeyote atakayefika kung'oa mabango yao.
Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alisema asingeweza kuwasiliana moja kwa moja na mwandishi wa Mwananchi lakini akaahidi kutuma taarifa ambayo hata hivyo haikujibu maswali ya msingi ambayo yanalalamikiwa na Askofu Kakobe.Ingawa taarifa hiyo haikugusia sababu za Tanesco kutotumia upande wa barabara ambao una nafasi kubwa na badala yake kubanana na makazi ya watu upande ambao kanisa hilo lipo, alisema Tanesco imefanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kwamba njia hiyo ya umeme haiwezi kumuathiri binadamu wala mazingira yake.Alieleza kuwa njia hiyo inapita kwenye eneo la hifadhi ya barabara na tayari wamepata kibali cha Wakala wa Barabara (Tanroads) kujenga njia hiyo ya umeme inayolenga kukidhi mahitaji ya umeme jijini ambayo yameongezeka kutokana na wingi wa shughuli za kibinadamu jijini.Alisema mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya Japani na unahusisha ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo 132kV kutoka Ubungo mpaka Makumbusho na kituo cha kupozea umeme Makumbusho."Shirika lingependa kuwataarifu wakazi wa maeneo hayo na wananchi kwa ujumla kuelewa kuwa hakuna madhara yoyote watakayopata wananchi wanaoishi na kupita maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme," alisema Badra na kuongeza:"Shirika la umeme lilifanya utafiti wa kina na wa kitaalamu pamoja na wa kimazingira kabla ya kuanza ujenzi wa mradi huo na Baraza la Taifa za Mazingira (NEMC) lilijiridhisha na kuridhia kuwa ujenzi huo hautakuwa na matatizo au madhara yoyote kwa wakazi au wapita njia wa maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme.
"Katika kufafanua namna njia hiyo itakavyojengwa ili wananchi wasidhurike, alisema nguzo zinazobeba umeme huo zinajengwa kwa urefu unaofuata viwango vya ujenzi wa msongo wa 132kV mijini ambavyo ni mita 23, akisema ndivyo vinavyokubalika kimataifa, na kuhakikisha usalama wa wakazi na wananchi katika maeneo hayo.Vile vile alisema mikono inayoshika vikombe vya waya za umeme katika nguzo hizo vitaelekezwa upande wa barabarani kwa umbali wa mita tatu kutoka kwenye nguzo."œShirika lingependa wananchi waelewe kuwa ujenzi wa njia hiyo ya umeme wa namna hiyo katika maeneo ya mijini ni teknolojia inayoendelea kutumika sehemu nyingine duniani mfano, Japani," alisema.

Source: Mwananchi

Thursday, January 7, 2010

Askofu Kakobe azuia Tanesco kupitisha nyaya eneo la Kanisa

ASKOFU mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zacharia Kakobe ameligomea Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitisha mbele ya kanisa lake njia ya umeme ya msongo mkubwa wa kilovolti 132.
Akofu huyo pamoja na mamia ya waumini wake, jana walikusanyika mbele ya kanisa hilo lililo kando ya Barabara ya Sam Nujoma karibu na Mwenge, jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kupambana baada ya kupata taarifa kwamba mafundi wa Tanesco wangewasili kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kupitisha njia hiyo ya umeme.
"Mimi nimejiandaa kuongoza waumini wangu katika kukabiliana na yeyote. Mimi nipo tayari kufa na nitahakikisha hawapitishi njia hiyo labda wawe wameniua," alilalamika.
Alilalamika kuwa iwapo umeme wa msongo huo utapitishwa eneo hilo utaathiri mitambo inayosaidia kunasa, kupaza na kurekodi sauti kwenye ibada zinazofanyika kanisani hapo pamoja na mpango wake wa kuanzisha kituo cha televisheni cha kanisa.
Isitoshe, alisema kwamba tayari Tanesco wamemuarifu kuwa itabidi wayang'oe mabango mawili ambayo yaligharimu Sh120 milioni ili kupisha mradi huo.
"Kama Watanzania haijatokea vita ya dini, basi ndiyo hii. Ni kubwa kuliko ile ya Wabarbeig," alisema Askofu Kakobe na kuitaka serikali iingilie kati suala hilo ili kuepusha dhahama inayoweza kutokea.
"Mimi na waumini wangu tumekubaliana tutakesha hapa usiku na mchana. Maana nasikia huwa wanaweza kuja usiku kubomoa mabango haya," alisema Askofu huyo mwenye maelfu ya waumini jijini Dar es Salaam.
Mwananchi lilipowasili jana eneo hilo ilikuta mamia ya waumini hao pamoja na Askofu Kakobe wakionekana kutokuwa na silaha yoyote lakini wakisisitiza kuwa wako tayari kwa vita dhidi ya mtu yeyote atakayefika eneo hilo kwa lengo la kung'oa mabango yao.
"Walifikiri kwa kuwa sisi ni walokole tutakaa kimya, lakini sisi tunasema katika hili hakuna cha kusema tutamwachia Mungu. Mungu yuko 'busy' (anakabiliwa na majukumu mengi) ana kazi nyingi, hili ni jukumu letu," alisema Askofu Kakobe.
Alilalamika kwamba utawala wa Rais Kikwete unalikandamiza kanisa lake huku akidai kuwa kama ingekuwa madhehebu mengine ya dini, kitendo kama hicho kisingetokea.
“Wanachokifanya hakina adabu! Kwa (askofu mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp) Pengo isingekuwa rahisi. Wanamuonea Kakobe kwa kuwa ni mnyonge,” alilalamika Kakobe akisema yuko tayari kufa ili mradi ahakikishe njia hiyo ya umeme haiwekwi karibu na kanisa lake.
Alibainisha kuwa awali njia hiyo ilikuwa ipite upande wa pili wa barabara mkabala na kanisa hilo, lakini wakazi wengi wa eneo hilo walipinga kitendo hicho hata pale walipoahidiwa kufidiwa.
"Hawa waliokataa, hata pale walipoahidiwa kufidiwa, wengi ni wasomi wa chuo kikuu. Eneo hilo ndilo lenye nafasi kubwa. Lakini wakaona upande huu hauna wasomi wanaweza kukubali kirahisirahisi tu.
Mimi katika hili nasema hapana," alisema Kakobe.
Kakobe alisisitiza kuwa yeye na waumini wake wameamua kuwa watakuwa wakikesha eneo hilo kuhakikisha watapambana na yeyote atakayefika kung’oa mabango yao.
Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alisema asingeweza kuwasiliana moja kwa moja na mwandishi wa Mwananchi lakini akaahidi kutuma taarifa ambayo hata hivyo haikujibu maswali ya msingi ambayo yanalalamikiwa na Askofu Kakobe.
Ingawa taarifa hiyo haikugusia sababu za Tanesco kutotumia upande wa barabara ambao una nafasi kubwa na badala yake kubanana na makazi ya watu upande ambao kanisa hilo lipo, alisema Tanesco imefanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kwamba njia hiyo ya umeme haiwezi kumuathiri binadamu wala mazingira yake.
Alieleza kuwa njia hiyo inapita kwenye eneo la hifadhi ya barabara na tayari wamepata kibali cha Wakala wa Barabara (Tanroads) kujenga njia hiyo ya umeme inayolenga kukidhi mahitaji ya umeme jijini ambayo yameongezeka kutokana na wingi wa shughuli za kibinadamu jijini.
Alisema mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya Japani na unahusisha ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo 132kV kutoka Ubungo mpaka Makumbusho na kituo cha kupozea umeme Makumbusho.
“Shirika lingependa kuwataarifu wakazi wa maeneo hayo na wananchi kwa ujumla kuelewa kuwa hakuna madhara yoyote watakayopata wananchi wanaoishi na kupita maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme,” alisema Badra na kuongeza:
“Shirika la umeme lilifanya utafiti wa kina na wa kitaalamu pamoja na wa kimazingira kabla ya kuanza ujenzi wa mradi huo na Baraza la Taifa za Mazingira (NEMC) lilijiridhisha na kuridhia kuwa ujenzi huo hautakuwa na matatizo au madhara yoyote kwa wakazi au wapita njia wa maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme.
Katika kufafanua namna njia hiyo itakavyojengwa ili wananchi wasidhurike, alisema nguzo zinazobeba umeme huo zinajengwa kwa urefu unaofuata viwango vya ujenzi wa msongo wa 132kV mijini ambavyo ni mita 23, akisema ndivyo vinavyokubalika kimataifa, na kuhakikisha usalama wa wakazi na wananchi katika maeneo hayo.
Vile vile alisema mikono inayoshika vikombe vya waya za umeme katika nguzo hizo vitaelekezwa upande wa barabarani kwa umbali wa mita tatu kutoka kwenye nguzo.
“Shirika lingependa wananchi waelewe kuwa ujenzi wa njia hiyo ya umeme wa namna hiyo katika maeneo ya mijini ni teknolojia inayoendelea kutumika sehemu nyingine duniani mfano, Japani,.. alisema.

Source: Mwananchi

Monday, January 4, 2010

Mchungaji Gwajima amjibu amtabiria kifo cha ghafla sheikh Yahya

Siku chache baada ya mtabiri mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussein wa Dar es Salaam kutangaza katika vyombo vya habari kuwa mwana CCM atakayejitokeza kuchuana na Rais Jakaya Kikwete katika kinyang’anyiro cha kugombea urais mwaka huu, atakufa ghafla, Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ Ubungo ametoa masharti matatu kwa mtabiri huyo vinginevyo naye atakufa ghafla.
Katika mahubiri kanisani hapo jana, Mchungaji Kiongozi, Gwajima alisema demokrasia ya Tanzania imo hatarini endapo mtu mmoja ataachiwa kuamua hatma ya taifa kinyume na mapenzi ya Mungu asiyekuwa na upendeleo kwa mtu yeyote.
“Baada ya kuendelea kutenda kazi zake zikiwa ni chukizo machoni mwa Mungu, leo ninatoa hukumu kutoka kwa Bwana, nanyi nyote mtachuja kuwa ni upi utabiri wa kweli kati ya Sheikh Yahaya na Mungu. Ninamwagiza Sheikh Yahaya afanye mambo matatu la sivyo naye atakufa ghafla kama alivyowatishia Watanzania wenzake,” alisema.
Sharti la kwanza alisema ni Sheikh Yahaya kwenda katika kanisa hilo la Glory of Christ na kuonana na mchungaji Gwajima yeye mwenyewe ili amwongoze kwa sala ya toba, kisha ampokee Yesu katika maisha yake.
Sharti la pili, Sheikh Yahaya ameamriwa kuanzia sasa aachane na utabiri wake ambao kwa miaka mingi alisema umewaumiza watu wengine wasiokuwa na hatia na kuwafaidisha wengine wachache kwa njia za giza.
Na sharti la tatu, Sheikh Yahaya ametakiwa, baada ya kuokoka, arudi katika vyombo vya habari kwa nguvu ileile aliyoitumia kutangaza utabiri wake wa mtu kufa ghafla na sasa awatangazie Watanzania mabaya yake yote aliyokwishayafanya kwa watu wa taifa hili hadi siku ya mwisho alipolazimika kuokoka.
Akifafanua juu ya masharti hayo, Mchungaji Gwajima alisema kimsingi yeye anamkubali Rais Jakaya Kikwete kuwa kiongozi wa taifa hili ila kinachomkera ni Sheikh Yahaya kuwatisha watu wengine wasitumie haki yao ya msingi katika kuikuza demokrasia hapa nchini.
Alipohojiwa kwa njia ya simu, Sheikh Yahaya ambaye alisema yuko nje ya jiji la Dar es Salaam kwa siku ya jana, alisema katika kipindi cha miaka 40 ya utabiri wake umekuwa sahihi siku zote na umaarufu wake ni wa kimataifa.
“Kamwe sitakwenda katika kanisa hilo, pia siko tayari kufuata sharti hata moja kutoka kwa mchungaji huyo.
Nimeanza utabiri kabla ya yeye kuwa shemasi wa kanisa hivyo endapo nitakufa najua ni siku zangu zimefikia mwisho wala si vinginevyo,” Sheikh Yahaya alisema.
Akitoa mifano ya utabiri wake ambao aliosisitiza kuwa sahihi mara zote, alitabiri msiba wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa kwa maelezo kwamba taifa litapata msiba mkubwa. Pia alisema aliwahi kutabiri kifo cha kiongozi mashuhuri ambaye kifo chake kingewakutanisha watu wa mataifa mbalimbali, dini, rangi na vyama mbalimbali vya siasa na kwamba kiongozi huyo alikuwa hayati Mwalimu Nyerere.
“Je, sikutabiri kuwa ndani ya CCM utazuka mtafaruku na kusababisha ufa ndani ya chama hicho kitu ambacho ninyi waandishi mmekishuhudia hivi karibuni?
Mimi siwezi kuongea kashfa yoyote dhidi ya mchungaji huyo bali ninachosema akipenda apeleke malalamiko yake Ikulu, kwani nako huko wapo watu wa kumjibu waliozishuhudia kazi zangu kwa miaka yote,” alitamba Sheikh Yahaya.
Alisema alitarajia kiongozi huyo wa kanisa aempe mwaliko rasmi waonane mahali popote siyo hapo kanisani ili waelezane masula ya nyota kwa undani badala ya ‘kumtisha’.
CHANZO: NIPASHE