HUWEZI KUMTUMIKIA MUNGU NA MALI
MATHAYO 6:24
"Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali."
Mali na Mungu wote ni mabwana wanaoweza kutumikiwa na wanadamu ila huwezi kuwatumikia wote kwa wakati mmoja. Ukitaka kuwatumikia wote lazima utamchukia mmoja na kuambatana na mwingine.
Ukiamua kuitumikia mali utafuata kile ambacho mali inataka ukifanye ili uipate na hata Kama kwa kufanya hivyo utamkosea Mungu. Vile vile ukitaka kumtumikia Mungu itakulazimu kufanya kile ambacho Mungu anataka ufanye hata Kama kwa kufanya hivyo utaikosa mali.
Kile ambacho Mungu atakutaka ufanye ukiamua kumtumikia na kile ambacho mali itakutaka ufanye ukiamua kuitumikia ni tofauti kabisa na Mara nyingi vitapingana ndo maana huwezi kumtumikia Mungu na Mali kwa wakati mmoja. Hawa ni waajiri wawili tofauti wenye mashariti yanayotofautiana kabisa.
Kwa mfano Mungu amesema tukiamua kumtumikia itatulazimu kutoa bure kile alichotupatia: yaani, tumepewa bure (vipawa, huduma) na tutoe bure. Mungu anatuagiza tutoe huduma bure bila kutoza pesa. Lakini Kama ukiamua kuitumikia mali itakutaka ufate kanuni zake ambazo ni kutoza pesa kwa Kila unachokitoa ili upate fedha au Mali zaidi.
HUWEZI KUMTUMIKIA MUNGU NA MALI LAKINI UNAWEZA KUMTUMIKIA MUNGU KWA MALI.
LUKA 8:2~3
na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
Moja ya sababu kwa nini Mungu huwa hawapati baadhi ya watoto wake Mali ni kuwa hawajui kutofautisha kumtumikia Mungu kwa mali na kumtumikia Mungu na mali. Kama huko tayari kumtumikia Mungu kwa mali basi hu-qualify kupewa Mali na Mungu maana ukizipata utaanza kuzitumikia na hivyo kuanzisha mgogoro na Mungu.
Money should be a tool to serve God and not a master of our lives. Kumbuka uzima wa mtu hauko ktk wing wa vita alivyonavyo
LUKA 12:15
Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
TAFAKARI, CHUKUA HATUA
2 comments:
Nikidhani utajiri umefananishwa na kiburi na unyanganyi. Yesu katika dunia hii alikuwa maskini na WAkristo wengine wameamini hivi ndivyo mambo ilivyo.
Kuna wakati mimi sijaamini kwamba Mungu anawezakunitajirisha. Hata hivyo, mawazo kama haya yakinijia, najikumbusha neno linalosema ya kwamba Mungu ndiye Muumba na mweza yote, hata pumzi ninayopumua ni kwa uwezo wake; hivyo basi, sistahili kumshuku.
Nikidhani utajiri umefananishwa na kiburi na unyanganyi. Yesu katika dunia hii alikuwa maskini na WAkristo wengine wameamini hivi ndivyo mambo ilivyo.
Kuna wakati mimi sijaamini kwamba Mungu anawezakunitajirisha. Hata hivyo, mawazo kama haya yakinijia, najikumbusha neno linalosema ya kwamba Mungu ndiye Muumba na mweza yote, hata pumzi ninayopumua ni kwa uwezo wake; hivyo basi, sistahili kumshuku.
Post a Comment