Thursday, August 29, 2013

BREAKING NEWS: ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA

BREAKING NEWS: ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA


Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo Gospel Kitaa imezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.
Source:http://gospelkitaa.blogspot.com/2013/08/breaking-news-askofu-moses-kulola.html

HII NDIO HISTORIA YA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA

HII NDIO HISTORIA YA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA

Marehemu Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake

MOSES KULOLA, aliyezaliwa mwaka 1928 katika familia ya watoto kumi, na kufariki mwezi Agosti 2013 katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam. Ambapo kwa sasa wamebaki ndugu zake wanne.

Moses Kulola alijiandikisha katika shule ya kwanza mnamo mwaka 1939. Shule hiyo ilikuwa inaitwa Ligsha Sukuma, ilikiwa ni shule ya Misheni. Baada ya kumaliza hapo Ligsha Sukuma Mission School, Moses Kulola akajiunga katika Idara ya  Uchoraji wa Majengo mnamo mwaka 1949. Na mwaka 1950 alibatizwa katika Kanisa la AIM Makongoro, mjini Mwanza.

 Alifanikiwa kumuoa Elizabeth na Mungu aliwajalia kupata watoto 10, ambapo kwa sasa saba (7) bado wako hai.  Alianza kazi za Umisionari mnamo mwaka 1950, ingawa alikuwa amesikia wito huo mwaka ule wa 1949!

Faustine Munishi(malebo) Moses Kulola,Emmanuel Mwasota.

 Mwaka 1959 aliajiriwa serikalini. Lakini pamoja na kuajiriwa huko Moses Kulola aliendelea na kuhubiri Injili katika Miji na Vijiji. Utumishi wake kama mwajiriwa wa Serikali ulikwisha mwaka 1962 baada ya kuwa amekabidhi nguvu, mwili na nafsi yake katika kazi ya Mungu! Ilipofika mwaka 1964 aliamua kusoma na akajiunga katika  Chuo cha Theolojia na kuhitimu katika kiwango cha Diploma mamo mwaka ule wa 1966.

Endelea kusoma historia hii kwa kubofya hapa chini 

Baada kupata Diploma hiyo hakuishia hapo bali aliendelea kusoma kwa Njia ya Posta na kupata Vyeti vingi sana kutoka Sehemu mbali mbali duniani.

Alitumikia miaka miwili kama mchungaji, 1961-1962, katika kanisa hilo la AIM na baada ya hapo akawa muumini wa Kipentekoste. Halafu akatumikia katika kanisa la TACR kuanzia 1966 hadi 1991 ambapo alijisikia kuanzisha Evangelistic Assemblie of God, maarufu kama EAGT. EAGT ni kanisa ambalo limefanikiwa kukua kwa kasi kubwa nchini hasa Tanzania, Zambia na Malawi ambapo jumla yake ni kama makanisa 4,000 yakiwa ni makanisa makubwa na madogo, na yeye Moses Kulola ndiye akiwa Askofu Mkuu na Msaidi wake akiwa Askofu Mwaisabira.

Ilikuwa sio  kazi rahisi kuendesha makanisa elfu nne (4,000) na ndiyo maana ikabidi Moses Kulola kuamua kugawanya makanisa hayo katika maeneo 34 ya kiutendaji, kukiwa na Kanda Tano ili kurahisisha kazi hiyo ya Mungu. Kila eneo na Kanda kuna mwangalizi wake.

R.I.P ASKOFU MOSES KULOLA

Source:http://pamojapure.blogspot.com/2013/08/hii-ndio-historia-ya-marehemu-askofu.html

MJUE MTUMISHI WA MUNGU ASKOFU MOSES KULOLA

MJUE MTUMISHI WA MUNGU ASKOFU MOSES KULOLA

Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.

Ni mume wa Elizabeth na wamezaa watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.

Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.

Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.

Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
Askofu Kulola aliyeketi akiwa na waimbaji wa injili nchini Mwinjilisti Faustin Munishi mkono wa kushoto pamoja na Emmanuel Mwasota. mwanzoni mwa mwaka 1970
Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake. 
 
Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana, katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola ni injili iliyonyooka na akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele bure.

Ukiacha mengi ambayo Mungu anaendelea kumtumia mtumishi wake huyu, kuna suala la nywele zake, askofu Kulola kama tulivyowahi kuandika siku zilizopita, hajanyoa nywele zake kwa takribani miaka 47 sasa, kwakuwa hakupendezwa na suala la kwenda salon kunyoa nywele zake hivyo akamwambia Mungu nywele alizokuwa nazo kwa wakati huo zisikue zaidi au kupungua, na ndivyo ilivyo mpaka sasa wembe haujapita kichwani mwake.
Askofu Kulola akipeana mkono na mwanae Daniel Kulola ambaye ni mchungaji.          






Historia ya Askofu Kulola yaandaliwa

Historia ya Askofu Kulola yaandaliwa

Taasisi isiyo ya kiserikali, inayojihusisha na utafutaji na ukusanyaji wa taarifa na shuhuda, ijulikanayo kama; Moses Kulola Faundation, imeanza kuandaa historia ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Dk. Moses kulola.
Histolia ya Askofu Kulola kwa ufupi, alizaliwa mwezi Juni 1928 katika familia ya watoto kumi. Alisomea shule ya msingi ya Ligsha Sukuma, halafu taasisi ya usanifu. Alibatizwa kikristo mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro. Alimwoa Elizabeth wakawa na watoto kumi.
Alifanya kazi ya uchungaji wa kanisa la AIC miaka ya 1961-1962 akaendelea na masomo ya kitheolojia. Baada ya kujiunga na dhehebu la kipentekoste alifanya kazi ya uchungaji ndani ya kanisa la TAG miaka ya 1966-1991. Akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa jipya mwaka wa 1991, kanisa la EAGT (kwa Kiingereza Evangelistic Assemblies of God) akawa askofu wao wa kwanza tangu mwaka uleule.
(Chanzo wikipedia)

Msemaji wa Shirika hilo Mwinjilisti Willy Kulola aliliambia gazeti la Kikristo la Jibu la Maisha siku chache zimepita kuwa lengo la kuandaa historia hiyo ni kutaka kuonyesha kazi kubwa ya Mungu aliyoifanya Askofu Kulola ya kuwaleta watu kwa Yesu.

Aliongeza kuwa mpakwa mafuta huyo wa Mungu ametimiza miaka 67 sasa tangu aanze huduma ya kumtumikia Mungu, huku akibainisha kuwa  kuna mafanikio makubwa yamepatikana ya kuvunja ngome za ibilisi katika maeneo mbalimbali ya taifa  ya Tanzania hata nchi za nje

“Katika hatua nyingine, ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na watanzania walio wengi  nchini na nje ya nchi ni kuwepo kwa maandishi ya kueleza huduma ya kiroho ya Mtumishi wa Mungu Dk. Moses Kulola,” alisema  Mwinjilisti huyo na kuongeza.

Hivi sasa mpakwa mafuta huyo wa Mungu metimiza miaka 67 tangu alipoitwa kumtumikia Bwana Yesu, kwa hiyo mchakato wa kuandaa historia ya baba yetu Dk. Kulola umeanza na utakamilika hivi karibuni.

Alisema lengo ni kumtukuza  Mungu kwa matendo makuu anayoyafanya kwa watu wake na kuangusha ngome za mwovu ibilisi, sambamba  na  kujipanga imara katika kuifanya kazi ya Bwana, ikiwa ni pamoja na kupata mbinu mpya  za kumkabiri shetani.
Askofu Dr Moses Kulo akiwa na kundi la wakristo wa Tanzania walipokuwa Israel

Source:http://gospelvisiontz.blogspot.com/2013/03/historia-ya-askofu-kulola-yaandaliwa.html