Thursday, August 27, 2009

Kardinali Pengo akemea wanasiasa kufundisha kazi maaskofu

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema maaskofu wasifundishwe namna ya kufikisha kazi ya Mungu na kufikisha ujumbe wao kwa waumini.
Kauli hiyo ya Pengo ambayo aliitoa mbele ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, pasipo kutaja waraka, imetolewa baada ya waraka uliotolewa na kanisa hilo kuzua mjadala mkali nchini, ukihusisha watu wa kada mbalimbali. Mjadala wa hoja hiyo pia ulifika katika Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM ambako ulijadiliwa na kutolewa maazimo.
Katika maazimio hayo, NEC iliwataka viongozi wa Serikali na Kanisa Katoliki kukutana, ili kupata ufumbuzi wa mzozo wa waraka huo ambao unataka wananchi wachague viongozi waadilifu wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani.
Mbali na NEC, wakati akijibu mwaswali ya papo kwa papo bungeni hivi karibuni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema ni vema uongozi wa kanisa hilo ukapeleka waraka huo serikalini, ili iweze kusambaza kwa wananchi, badala ya utaratibu wa sasa unaotoa mwanya kwa kila dhehebu kujiandikia na kusambaza nyaraka.
Akiendesha misa ya ibada takatifu ya kumuombea marehemu Askofu Mkuu Anthony Mayalla wa Jimbo Kuu la Mwanza, kwenye viwanja vya Kawekamo, Pengo alisisitiza, hawatakiwi kufundishwa namna ya kuandika barua kwenda kwa waumini wao, kwa sababu kufanya hivyo ni kuwafanya maaskofu hao washindwe kufikisha neno la Mungu kwa waumini
wao.
“Katu kanisa halitaruhusu maaskofu kuandika Barua na kuipeleka kwanza serikalini ikajadiliwe ndipo iruhusiwe kwenda kwa waumini. Kama itakuwa hivyo ni heri maaskofu hao wakaacha kabisa kufanya chochote,” alisisitiza.
Pengo alisisitiza kuwa suala la kuambiwa wanapotaka kuwasiliana na waumini wao kuwasiliana na chama (CCM) na serikali kwanza ni kuwapeleka waumini sehemu isiyostahili, hivyo kanisa haliko tayari kukubaliana na suala hilo.
Kadinali Pengo alisema maaskofu waachwe wafanye kazi yao pasipo kuingiliwa na mtu yoyote na kwamba, kanisa haliko tayari kuwaruhusu maaskofu kuandika barua kwa waumini na kuipeleka kwanza serikalini ama kwenye chama kwa ajili ya kujadiliwa.
Mjadala wa Waraka wa Kanisa Katoliki ulichochewa zaidi na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru, katika Bunge la Bajeti mwaka huu baada ya kutaka kanisa hilo liuondoe kwa waumini kwasababu umejaa uchochezi wa kidini.
Kingunge baada ya kujibiwa na maaskofu, aliibuka tena akitaka kuombwa radhi kwa madai kuwa alishushiwa heshima kwa kumlinganisha na mafisadi.
Katika hatua nyingine Kadinali Pengo aliwaonya watu wanaopiga

Source: mwanachi

No comments: