Hii ni Blogu ya watu wote...uwe huru kuchangia neno lolote unaloona linafaa kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo
Thursday, August 29, 2013
HII NDIO HISTORIA YA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA
HII NDIO HISTORIA YA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA
Marehemu Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake
MOSES KULOLA, aliyezaliwa mwaka 1928 katika familia ya watoto kumi, na kufariki mwezi Agosti 2013 katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam. Ambapo kwa sasa wamebaki ndugu zake wanne.
Moses Kulola alijiandikisha katika shule ya kwanza mnamo
mwaka 1939. Shule hiyo ilikuwa inaitwa Ligsha Sukuma, ilikiwa ni shule ya
Misheni. Baada ya kumaliza hapo Ligsha Sukuma Mission School, Moses
Kulola akajiunga
katika Idara ya Uchoraji wa Majengo mnamo mwaka 1949. Na mwaka 1950 alibatizwa katika Kanisa la AIM Makongoro, mjini Mwanza.
Alifanikiwa kumuoa Elizabeth na Mungu aliwajalia
kupata watoto 10, ambapo kwa sasa saba (7) bado wako hai. Alianza kazi
za Umisionari mnamo mwaka 1950, ingawa alikuwa amesikia wito huo
mwaka ule wa 1949!
Mwaka 1959 aliajiriwa serikalini.
Lakini pamoja na kuajiriwa huko Moses
Kulola aliendelea na kuhubiri Injili
katika Miji na Vijiji. Utumishi wake kama mwajiriwa wa Serikali
ulikwisha mwaka 1962 baada ya kuwa amekabidhi nguvu, mwili na nafsi
yake katika kazi ya Mungu! Ilipofika mwaka 1964 aliamua kusoma na akajiunga katika Chuo cha Theolojia na kuhitimu katika kiwango cha
Diploma mamo mwaka ule wa 1966.
Endelea kusoma historia hii kwa kubofya hapa chini
Baada kupata Diploma hiyo hakuishia hapo
bali aliendelea kusoma kwa Njia ya Posta na kupata Vyeti vingi sana
kutoka Sehemu mbali mbali duniani.
Alitumikia miaka miwili kama mchungaji,
1961-1962, katika kanisa hilo la AIM na baada ya hapo akawa muumini wa
Kipentekoste. Halafu akatumikia katika kanisa la TACR kuanzia 1966 hadi
1991 ambapo alijisikia kuanzisha Evangelistic Assemblie of God, maarufu
kama EAGT. EAGT ni kanisa ambalo limefanikiwa kukua kwa kasi kubwa
nchini hasa Tanzania, Zambia na Malawi ambapo jumla yake ni kama makanisa
4,000 yakiwa ni makanisa makubwa na madogo, na yeye Moses Kulola ndiyeakiwa Askofu Mkuu na Msaidi wake akiwa Askofu Mwaisabira.
Ilikuwa sio kazi rahisi kuendesha makanisa elfu
nne (4,000) na ndiyo maana ikabidi Moses Kulola kuamua kugawanya makanisa hayo katika maeneo 34 ya
kiutendaji, kukiwa na Kanda Tano ili kurahisisha kazi hiyo ya Mungu.
Kila eneo na Kanda kuna mwangalizi wake.
No comments:
Post a Comment