“Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.” (1Timotheo 2:1-6) “Nami Nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana Mungu” (Ezekiel
22:30,31).
Bwana Yesu asifiwe wapendwa!
Tunamshukuru sana Mungu kwa neema na rehema zake katika nchi yetu na pia tunamshukuru kwa ajili ya blog hii,tunaamini yapo makusudi yake hapa.
Ndugu zangu, Mungu ameweka ndani ya moyo wangu haja/mzigo wa kuomba kwa ajili ya nchi hii,hasa kwenye maeneo yanayohusu siasa na uongozi wa serikali yetu. Lakini pia nimegundua na kumshukuru Mungu kuwa ameweka mzigo kama huu kwa watu wengine wengi pia,namshukuru Mungu kwa hilo.
Tumekusudia kuanziasha mtandao wa watanzania walio ndani na nje ya Tanzania kwa ajili ya kushika zamu zetu kumwomba Mungu kwa ajili ya nchi hii.Tumekusudia kuuita Tanzania Prayer Network (TNP) (*Bado tunakaribisha maoni kuhusu hili jina).Mtandao huu utakuwa na majukumu yafuatayo;
a) Kuomba toba kila siku kwa ajili ya maovu yafanyikayo nchini kwetu hasa na viongozi na wanasiasa.
b) Kuwaombea viongozi wa serikali na wa vyama vya siasa kila siku ili Mungu awasaidie.
c) Kuchukua hatua ya kuwashauri viongozi wa serikali na siasa juu ya mambo muhimu katika nchi yetu.
d) Kuchukua jukumu la kuingia katika uongozi wan nchi hii kwa wale wenye upako huo.
e) Kuchukua jukumu la kuonyesha mfano bora kwa viongozi pale tulipo.
Majukumu mengine tutaendelea kufahamishana.
Tunawakaribisha na kuwasihi “wapendwa” watanzania popote walipo tuungane kwa ajili ya hili.
Kama upo tayari kwa ajili ya hili, basi tutumie email yenye maelezo yako kama Jina,Mahali unapoishi,Kanisa unalosali,mtazamo wako juu ya hili n.k ,Tuma email hiyo kwa;
savedlema@yahoo.com -Tanzania,
chalujohn@yahoo.com -Brother Chalukulu,Norway,
hkalenga@mirarco.org -Brother Kalenge,Canada
Tuache kulalamika,tushike zamu zetu kuomba.Karibuni.
Mungu awajaze nguvu zake.
No comments:
Post a Comment