Monday, April 28, 2008

Mbaroni kwa kumbaka mke wa mchungaji

JESHI la polisi mkoani Shinyanga, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kumbaka makaburini mke wa mchungaji wa kanisa moja la kikristo wilayani Bukombe, Mkoa Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Shaibu Ibrahim, alisema tukio hilo limetokea Aprili 21 mwaka huu majira ya saa nane usiku katika pori la makaburi, umbali wa kilomita 2 kutoka katika makazi yake yaliyopo majengo mapya, Kata ya
ushirombo wilayani humo.
Alisema siku hiyo ya tukio, watu hao walivamia nyumba ya mchungaji aliyefahamika kwa jina moja tu la Siafrika, wa Kanisa la Evangelism Living, ambaye
hakuwepo siku hiyo baada ya kuvunja mlango wa nyumba yake kwa fatuma na kumkuta mke wake mwenye umri wa miaka 35.
''Baada ya kuingia ndani watu hao walidai wapatiwe fedha na mwanamke huyo aliwapatia Shs10,000 hata hivyo, walimchukua na kumpeleka katika pori la makaburini umbali wa kilomita 2 kutoka nyumbani kwake na kuanza kumbaka kwa zamu,''alisema kamanda Ibrahim.
Aliwataja watu wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa wote ni wakazi wa Kilimahewa mjini Ushirombo na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi upelelezi dhidi yao utakapokamilika.
Katika tukio jingine, watu wanaodhaniwa kuwa ni sungusungu wa kijiji cha Bugege
wilayani Bukombe, wazichoma moto nyumba nne za wanakijiji wenzao, wakiwatuhumu
kujihusisha na vitendo vya ujambazi.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, brahim, alisema tukio hilo limetokea Aprili 21, mwaka huu majira ya saa 6 usiku.
Aliwataja waliochomewa nyumba zao kuwa ni pamoja na Fredrick Mageni, Mlondela
Lusiba, Masumbuko Michael na Timotheo Joseph, wote wakazi wa kijiji cha
Bugege.
Kamanda Ibrahim aliongeza kwa kusema kuwa sungusungu hao walichukua uamuzi huo baada ya watuhumiwa hao kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuvunja nyumba ya mwanakijiji mwenzao, Method Tulinge, siku za nyuma na mlalamikaji hakufika mahakamani kutoa ushahidi, jambo lililowawanya waachiwe huru kitendo kilichowachukiza wananchi hao na kuamua kuzichoma moto nyumba zao.
Hata hivyo, Kamanda huyo alisema wakati wa tukio hilo watu hao hawakuwemo ndani ya nyumba hizo na hasara kamili ya mali zilizoteketea, bado haijajulikana.
Source: Mwananchi

1 comment:

Anonymous said...

Hawatakuwa salama hao jamaa na tamaa zao, lazima Mungu afanye jambo katika hili , KAMA NA KAMA TU HAO JAMAA, hawakuwa na lengo la kulipiza kisasi.

Ni tukio lisilo la kawaida maana kwa uzoefu wangu majambazi wengi huwa wanaogopa wachungaji wakijua watauawa.

Katika dunia ya leo ambayo tuna wachungaji wengi,wako ambao wanalala au wanatembea na wake za watu!! ikitokea hivyo wachungaji hata muitwe dunia nzima kuwa wachungaji kama hamja simama, malipo ni hapa hapa.

Nina imani huyu ni mtumishi mzuri wa Mungu, nina imani pia, Mungu kuulinda ufalme wake, hatakubali kabisa swala hili, hao jamaa pengine hata kabla ya mahakamani basi lazima wafe !!! wamegusa mboni ya Mungu.