Tuesday, September 29, 2009

Maelfu wajitokeza kumuaga Mchungaji Masalu

Maelefu ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, jana walijitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa mchungaji wa Temeke EAGT , Karisti Masalu aliyefariki dunia na kutangulia mbele za Bwana YESU alhamisi iliyopita saa 3 na nusu usiku hapa jijini Dar es Salaam.

Umati wa Maaskofu,wachungaji,mitume na watumishi mbalimbali wa Mungu pamoja na wananchi mbalimbali walijitokeza kwa wingi jana tangu asubuhi na jioni kabisa kuhudhuria ibada hiyo iliyokuwa imejaa furaha na simanzi kwa pamoja.

Muongozaji wa ibada hiyo mchungaji Mwanjala wa Sinza EAGT kabla ya kusoma wasifu wa marehemu aliwakaribisha maaskofu na wachungaji mbalimbali maarufu walimfahamu na kuzaliwa chini ya huduma ya mtumishi wa Mungu Masalu ili waweza kutoa wosia.

Baadhi ya waliotoa nasaha kuhusu marehemu alikuwa ni Askofu Zakary Kakobe,Mtume Dustan Maboya,Mch. Anthony Lusekelo,Askofu Kameta,Askofu Shemsanga,Makamu wa Askofu mkuu wa EAGT mzee Mwakisyala aliyehubiri na wengine wengi wengi.Wote hao walieleza jinsi walivyozaliwa kihuduma kutokana na huduma ya Mch. Masalu.


Wengi walikiri kuwa kanisa la Temeke ndilo hasa kiini cha upentekoste hapa jijini Dar es Salaam.

Huduma nyingi kubwa hapa jijini Dar zimetokana na huduma ya mtumishi huyu wa Mungu.

Pastor Masalu atakumbukwa kwa moyo wake wa kujitolea na unyenyekevu wa hali ya juu kiasi kwamba hakuna anayebisha kuwa mtu huyu alikuwa ni mtu wa Mungu.Hakuwa na makuu wala makundi.Unyenyekevu wa Mch. Huyu uliwapa changamoto wengi waliofika kanisani hapo.

Mlima sayuni ulikuwepo eneo la tukio na kufanikiwa kuchukua picha kazaa za matukio ya msiba huo.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa ,jina la Bwana libarikiwe





No comments: