Hivi majuzi mwanamme huyo kaamua na kubeba mimba kwa niaba ya mke wake kwa kujipandikizia mimba mwilini mwake baada ya kununua manii za kiume toka benki moja huko Marekani. Kwa sasa inasemekana mwanamme huyo anatarajia kujifungua mwezi juni, mwaka huu. Mimba hii ni katika jaribio lake la pili, ikiwa ya kwanza iliyoharibika ambayo alikuwa ni ya watoto watatu na ilitungwa nje ya mfuko wa uzazi ambayo pia ilipelekea kufanyiwa upasuaji uliosababisha kwa yeye kupoteza via vya uzazi jinsia ya kike upande wa kulia. Akihojiwa, kaka yake alifurahia kuharibika huko alijibu akionesha kutofurahishwa na tendo hilo kwamba ni afadhali imekuwa hivyo, kwani nani ajuaye kama ingelizaliwa mizimu???
Mwanamme huyo bandia anaifurahia hali hiyo na tayari ana mipango ya kununua nyumba yeye pamoja na mkewe ili waendelee kumlea mtoto wao mtarajiwa kwa pamoja kama familia! Japo anapata upinzani mkubwa kutoka kwa madaktari, manesi na hata jamii inayomzunguka kwa kitendo chake hicho kinachoonekana dhahiri kuvuka maadili na miiko ya kibinadamu!
Kwa hali kama hii, je tutaipona hasira ya Mungu hapa duniani? Mungu akiamua kumuadhibu mwanadamu kwa maovu yake je tuna sababu ya kujitetea mbele zake? Kwani nini moyo wa mwanadamu umejawa na kuwaza maovu siku zote? Ee Mungu wa mbinguni twahitaji rehema zako utuepushe na maovu haya, na uwasamehe wote wanaokwenda kinyume nawe kwa kuwarejesha kwako kwa roho yako ya rehema na upendo ambao ndio asili yako!
4 comments:
aisee hii habari inasikitisha sana.naona sasa wazungu wanataka harira za Mungu ziwawakie huko.
Eeh Mungu tuepushe na uovu huu.
BabA ChiNYeMi
vituko vya namna hiyo ni vya kawaida huko kwa wenzetu.
angalia hapa
http://www.malepregnancy.com/
http://www.huffingtonpost.com/2008/03/26/pregnant-man-fin_n_93488.html
haya mambo yatakuja TZ, wabongo kuiga mambo. hawa manesi wanamlalamikia kitendo chake cha kubeba Mimba, wanakosea hakuanza leo matatizo, alianza tangu aliposema anataka kuwa mwanaume!!!! it is too late, tamaa ikichukua mimba hubeba dhambi.
Jamani tuombeni hii hali inasikitisha achilia mbali kuudhi,
Paulo alitaka awachape bakora watu fulani, huyu naye naona kama namwona vile, nimpige kofi la kilokole(kama lipo) kofi la wivu wa KiMungu.
Your blog keeps getting better and better! Your older articles are not as good as newer ones you have a lot more creativity and originality now keep it up!
Post a Comment