Monday, September 24, 2007

Unakumbuka hizi picha?
Siku Mzee Moses Kulola (Askofu mkuu wa EAGT) alipokumbatiana na Mzee Emmanuel Lazaro wa TAG pale kanisani Full Gospel kwa Askofu Kakobe.
Siku hii ilikuwa ni siku maalum ya kupatana kwa maaskofu wetu hawa wawili baada ya utengano wa muda mrefu wa kanisa la TAG na EAGT.Japokuwa siku hii watumishi hawa wa Mungu walisema hawakuwa kuwa na ugomvi wowote kati yao ila watu ndio walikuwa wakiwazushia.Walikumbatiana kwa furaha sana na hao wawili ni wake zao wakikumbatiana pia kwa furaha.

Picha hii hapa chini ni Mwimbaji wa injili wa siku nyingi Mtanzania anayeishi Kenya Faustin Munishi akiwa na Mchungaji Mwasota wakipiga picha na Askofu Moses Kulola enzi hizi injili ilikuwa si ya mzaha kama ilivyo sasa kuna wasanii wengi wamejiingiza makanisani.Picha hii ilipigwa miaka ya mwishoni mwa sabini au mwanzoni mwa themani.Mchungaji mwosota pia alikuwa ni mwimbaji maarufu hasa kwenye mikutano ya mzee kulola.Hata leo hii wote wawili Munishi na Mwasota bado wanaimba na niwachungaji.

2 comments:

Anonymous said...

Aisee hii picha ya mzee Kulola wakati hajawa mzee kama alivyo sasa imenifurahisha sana,nimefurahi kumwona baba yangu wa kiroho.Huyu mzee amefanya sana kazi ya Mungu huko nyumbani Tanzania.Mungu ambariki sana.

Pastor Victor M.
Dallas

Godhold said...

Mtumishi Kulola amefanya kazi kubwa ya injili Nchini kwetu na kwingineko. Mungu ambariki kwa matunda aliozaa kila mahali.Nitafurahi kuona siku moja wafanye mkutano pamoja na askofu Lazaro na watumishi wengine waweze kuweka mwili wa Kristo pamoja Tanzania.