Thursday, March 21, 2013

Tamko la Maaskofu

Tamko la Pamoja la Maaskofu wa madhehebu yote nchini Tanzania kuhusu masuala ya Uchinjaji na hali ya usalama wa nchi

Kutoka Kushoto: Askofu David Batenzi (PCT), Askofu Tarcisius J. M. Ngalalekumtwa (TEC) na Askofu Peter Kitula(CCT).
JUKWAA LA WA WAKRISTO TANZANIA (TCF)

“ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI, NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA” (Lk.2:14)TAMKO LA PAMOJA LA MKUTANO MKUU WA DHARURA WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA


1.Utangulizi


Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) linajumuisha Taasisi Kuu za Makanisa nchini kama ifuatavyo:-

Jumuiya ya Kikristo Tanzania – CCT
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania – TEC
Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania – PCT
Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA (Watazamaji)
Katika Mkutano wake Mkuu wa Dharura uliofanyika katika Kituo cha Mikutano na Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini, Jijini Dar es Salaam, tarehe 8 Machi, 2013; 

Wajumbe walitafakari kwa undani juu ya kuzorota kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini Tanzania, pamoja na mauaji na mashambulizi ya viongozi wa dini; na hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya uhalifu huo unaotekelezwa na Waislamu wachache. Katika taswira hiyo, Kanisa lilitathmini juu ya wajibu, utume, na sauti yake ya kinabii kwa taifa letu kuhusiana na mambo hayo. 

2. Hali halisi ilivyo hivi sasa hapa nchini kwa mtazamo wa Kanisa
Ushahidi wa kihistoria na kimazingira unaonyesha wazi kuwa kwa sasa Kanisa nchini Tanzania limo katika kipindi cha mateso ya kimfumo (systematic persecution), kama vipindi vingine 10 vya mateso katika Historia ya Kanisa hapa duniani. 


Pamoja na mateso haya ya kimfumo, tunatambua wazi kuwa wanaotekeleza haya ni kikundi kidogo tu cha Waislamu wa Tanzania, kama wale wengine wa Barani Afrika (k.m. Boko Haram kule Nigeria). Waislamu walio wengi hawafurahii mambo yanayotokea. Wao pia wanaitazamia Serikali kuthibiti hawa wachache wanaochafua dini ya Kiislamu na kuwafanya Waislamu wote waonekane kuwa maadui wa Ukristo, jambo ambalo siyo kweli. 

Kutokana na hali hiyo, mkutano mkuu wa dharura wa Jukwaa la Wakristo umeyaangalia maeneo makuu yenye migogoro ikiwa ni pamoja na:


2.1. Mgororo wa nani anastahili kuchinja kitoweo Hivi karibuni hapa nchini tumeshuhuduia mgogoro juu ya uchinjaji wa mifugo ambayo nyama yake inapaswa kuuzwa kwa watu wa imani mbalimbali wakiwemo Wakristo na Waislamu. Tunafahamu kwamba sheria ya nchi yetu inaweka bayana juu ya usalama wa nyama hizo kiafya, lakini sheria haielekezi kuwa dini fulani ndiyo waumini wake wanapaswa kuchinja mifugo hiyo. 


Kwa misingi hiyo Kanisa linatamka kuwa:-

a) Hoja ya dini moja kudai kuhodhi (exclusive right) uchinjaji wa mifugo kwa misingi ya imani yake ni kinyume cha haki ya uhuru wa kuabudu ambayo amepewa kila mtu ndani ya nchi hii kikatiba katika Ibara 19. 


b) Kwa kuwa kuchinja wanyama na ndege ni Ibada kwa Waislamu, Kanisa litambue na kuheshimu jambo hilo. Lakini pamoja na kutambua haki ya Waislamu kujichinjia wanyama na ndege kama Ibada kwao, Wakristo wasilazimishwe kula nyama zilizochinjwa kwa misingi ya Ibada za Kiislamu. Kwa kuwa wananchi wa Tanzania ni wa dini mbalimbali na mila za makabila mbalimbali, tunaitaka Serikali itamke wazi kuwa kila raia ana uhuru wa kufuata imani yake katika suala la uchinjaji. 


c) Kuhusiana na jambo hili tunashindwa kabisa kuelewa msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali. 


Wakati wa Serikali ya awamu ya pili chini ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Muislamu, ulipotokea ugomvi wa mabucha ya nyama ya nguruwe Dar es Salaam, Rais huyu Mstaafu kwa kulinda Katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda, alisema mwenyewe kwa nguvu zote kuwa kila mtu ana uhuru wa kula anachotaka na mtu wa dini moja asimhukumu mtu wa dini nyingine kwa kile anachokula. 

Baada ya Rais Mstaafu kukemea jambo hili, hali ikawa ya amani na utulivu. Kwa nini Serikali yetu ya sasa inapata kigugumizi kuhusiana na suala zima la nani achinje?

d) Kwa mantiki hiyo hapo juu katika kipengele cha a-c, Wakristo wanaitaka Serikali iweke utaratibu wa kugawana machinjio na mabucha kati ya Wakristo na Waislamu ili kila Mtanzania awe huru kujinunulia kitoweo mahali anapotaka. 


Sambamba na kuitaka Serikali kufanya hivyo, tunawakumbusha Wakristo wote Tanzania kuelewa kuwa watakuwa hawajavunja sheria yoyote ya nchi wakiamua kujichinjia kitoweo chao wenyewe. Kuhusiana na tangazo hili kwa Wakristo wote, tunaitaka mihimili ya dola (Serikali na Mahakama) kuheshimu Katiba ya Nchi yetu, na kipekee kuhusiana na jambo hili Ibara ile ya 19.

e) Kwa upande mwingine, kwa kuwa tayari zipo bidhaa za vyakula katika nchi hii ambazo zina nembo ya ‘halal’ na nyingine hazina nembo hiyo, huu ni uthibitisho kuwa vyakula hivyo vimegawanywa kwa kufuata misingi ya imani za kidini. Kwa hiyo, madai ya kugawanya machinjio na mabucha kwa kufuata misingi ya dini sio jambo jipya kwa sasa katika nchi hii.


2.2 Uchomaji wa Makanisa ulioambatana na vitisho na mauaji ya viongozi wa KanisaKanisa linalaani vikali mauaji ya kidini yanayoendelea kufanywa pamoja na vitisho (systematic persecution) kwa viongozi wa Kanisa na Wakristo wote kwa ujumla. 


Mtiririko wa matukio mbali mbali ya nyuma yanatudhihirishia kuwa kumekuwepo na mpango wa muda mrefu wa haya yanayotokea sasa hivi. Tarehe 15 Januari 2011, kundi la Waumini wa Kiislamu walipokutana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, miongoni mwao walikuwamo mashehe, walijadili hali ya nchi ya Tanzania kuongozwa kwa mfumo wa kidini. Mkutano huo ulihitimishwa kwa kutoa tamko dhidi ya kile kilichoitwa mfumo Kristo katika nchi yetu! 


Japo Serikali na vyombo vyake vya usalama wa Taifa vimekuwa vikipata taarifa za vitisho dhidi ya viongozi wa Kanisa, mauaji, kuchomwa kwa nyumba za ibada, pamoja na maneno ya uchochezi kupitia mihadhara, vipeperushi, CD na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taasisi zinazofahamika, hata hivyo Serikali kwa kiasi kikubwa imeshindwa kuchukua hatua kwa wakati muafaka na wanasubiri hadi maovu yatendeke ndipo ati waanze kufanya uchunguzi. 


Kwa Serikali yetu inaonekana wazi kuwa katika hili ile methali kwamba “Kinga ni bora kuliko tiba” haina maana yoyote. Hii ni kuonyesha udhaifu mkubwa wa vyombo vya usalama wa Taifa au pia kwamba vyombo hivi vinafurahia kutoweka kwa amani nchini mwetu, jambo ambalo linalifanya Kanisa nchini Tanzania liamini kwamba matukio haya yanayoendelea kutokea ni dalili kuwa Serikali ina agenda ya siri dhidi ya Ukristo.
Kutokana na hayo Jukwaa la Wakristo Tanzania linatamka kama ifuatavyo:


a) Tunatambua kwamba ni jukumu la Serikali kuwatendea raia wake kwa usawa na bila ya ubaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 12 na 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Viongozi wa Kanisa wanatamka kwamba Serikali imeshindwa kuheshimu Katiba juu ya hizi haki za raia wake na kupelekea waamini wa dini ya Kikristo kukosa imani na Serikali iliyoko madarakani, hasa kuhusu ulinzi na usalama wao na mali zao kama inavyoagizwa kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. 

Kama Serikali inaona haiwezi kuwahakikishia wananchi usalama wa uhai wao na mali zao, na hivyo kuwafanya waishi maisha ya hofu inayotokana na vitisho, basi kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, hakuna sababu ya Serikali iliyoko madarakani kung’ang’ania kuongoza nchi. 

b) Kwa kuwa ulinzi wa raia ni haki ya kikatiba na kisheria, Serikali inatakiwa iwalinde raia wake. Kama Serikali imeshindwa kuwalinda raia wake, Kanisa linataka Serikali ikiri hivyo ili Kanisa liwaambie wananchi waiwajibishe Serikali na Viongozi wanaoifanya Serikali ishindwe kutimiza wajibu wake. 


Jukwaa la Wakristo linasema:
Kama Serikali haitachukua hatua za makusudi dhidi ya mambo haya yaliyoainishwa hapo juu, Kanisa litachukua hatua ya kuwaambia waamini wake kwamba Serikali iliyoko madarakani inaibeba dini moja, na hivyo Kanisa litatafakari upya uhusiano wake na Serikali. 


3. Wakristo walioko Zanzibar
Wakristo walioko Zanzibar wanatishiwa maisha yao na mali zao zinaharibiwa mara kwa mara, kiasi cha wengine kuamua kuhamia Tanzania Bara. Kigezo cha unyanyasaji huo ni suala la udini na muungano. Inaonekana ni kama vile Watanzania waliozaliwa Bara hawana haki ya kuishi Visiwani. 


Na kumbe wale waliozaliwa Visiwani wafikapo Barani wana haki zote. Kanisa linaitaka Serikali iwahakikishie Wakristo walioko Zanzibar usalama wao na wa mali zao maana hiyo ni haki yao ya Kikatiba. 

4. Vitisho na mauaji ya Wanakanisa
Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ichukue hatua za makusudi za kuzuia vitisho na mauaji kwa Viongozi wa Kanisa na Wakristo kwa ujumla. Vinginevyo Kanisa litautangazia ulimwengu kuwa Tanzania ni nchi mojawapo inayovunja haki za binadamu kwa ubaguzi wa kidini na kulitesa Kanisa kimfumo. 


5. Matumizi ya Vyombo vya Habari:
Kwa kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimeruhusu vitumiwe kuwatukana Viongozi wa Kanisa, tunatoa nafasi kwa vyombo hivyo kuomba radhi; vinginevyo tutaitaka dunia ivielewe kuwa navyo ni sehemu ya chanzo cha migogoro. 


Pia tunachukua nafasi hii kuvitahadharisha vyombo mbalimbali vya habari kupima kwa kina ni nini kinachosemwa na viongozi wa kidini ili kuviepusha vyombo hivyo kutumika kwa nia ya uchochezi; yasije yakatukuta kama yale yaliyotokea kule Rwanda 1994. 

6. Hitimisho:
Kanisa linaendelea kusisitiza kuwa silaha kuu ya Mkristo katika nyakati hizi ni maombi na kufunga. Kwa mantiki hiyo, Kanisa linawataka Wakristo wote nchini Tanzania kuungana kwa pamoja katika maombi na kufunga kwa muda wa siku saba kwa ajili ya hali hii iliyojitokeza hapa nchini. Maombi hayo na mfungo vifanyike kabla ya Pasaka, yaani kuanzia, tarehe 24/3/2013 hadi 30/3/2013. 


Kwa niaba ya Maaskofu 177 walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Dharura wa Jukwaa la Wakristo na kutoa maazimio hayo.
1. Askofu Peter Kitula – Mwenyekiti CCT
2. Askofu Tarcisius J. M. Ngalalekumtwa Rais TEC
3. Askofu David Batenzi Mwenyekiti PCT


Source: http://mjapinc.blogspot.com/2013/03/tamko-la-pamoja-la-maaskofu-wa.html?spref=fb

Tuesday, March 19, 2013

Pastor Peter Mitimingi Mexico

 Pichani ni mkurugenzi wa taasisi ya kidini ya Voice of Hope Ministries,Mchungaji Peter Mitimingi akiwa katika huduma huko Mexico City ,Mexico mapema mwezi huu.Mungu alimtumia kwa namna ya kipekee sana...Taasisi ya Voice of Hope ni moja kati ya taasisi ambazo zimekuwa zikifanya kazi kwa karibu sana na Kampuni ya DigitaBrainSaturday, March 16, 2013

Pastor Peter Mitimingi

Ni mmoja kati ya wachungaji ninaowafahamu kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita ambao Mungu amewainua sana kihuduma,kiupako,kijamii na kifedha.Pichani ni picha za pastor Mitiminig akiwa Marekani kwa shughuli za kihuduma.Hapa akiwa katika ndege ya kukodi kutoka Mexico kwenda Califonia kwa ajili ya kuwahi mikutano mingine ya injili.Kwa jinisi ninavyomfahamu naweza kusema kwa dhati kabisa kuwa hakika Mungu anainua na kubariki watu wake.


Friday, March 8, 2013

Ahmadinejad's claim that Chávez will be resurrected with Jesus 'went too far'

Iranian president's tribute to late Venezuelan president criticised by some of his country's influential clerics as against Shia Islam
Mahmoud Ahmadinejad with Hugo Chávez in 2012
Mahmoud Ahmadinejad with Hugo Chávez in 2012. The Venezuelan president was one of the Iranian leader's closest allies.
Iran's president, Mahmoud Ahmadinejad, has been criticised for saying that Hugo Chávez will be resurrected along with Jesus Christ in his tribute to the Venezuelan president who died on Tuesday.
Ahmad Khatami, an influential cleric in the country's assembly of experts, said on Wednesday that Ahmadinejad went "too far" with his claim that Chávez would "return on resurrection day".
"I say directly that he went too far with what he mentioned in his tribute," said Khatami, who is a Tehran Friday prayer leader and a close ally of Iran's supreme leader, Ayatollah Ali Khamenei. "The president is well aware that such a tribute will provoke reactions in our religious institutes … He could have sent a diplomatic message with no religious connotations."
On Wednesday, the Iranian cabinet declared a day of national mourning, and Ahmadinejad wrote a letter of condolence addressed to Venezuela's interim president, Nicolás Maduro.
"Chávez is alive, as long as justice, love and freedom are living. He is alive, as long as piety, brightness, and humanity are living," he wrote, according to the English translation of the letter published by the semi-official Mehr news agency.
"He is alive, as long as nations are alive and struggle for consolidating independence, justice and kindness. I have no doubt that he will come back, and along with Christ the Saviour, the heir to all saintly and perfect men, and will bring peace, justice and perfection for all."
The president did not name Imam Mahdi, the revered saviour of Shia Islam, in his tribute, but by naming Christ he made clear that Chávez would also be among the Imam's allies. The reappearance of Mahdi is anticipated by believers in a manner comparable to that with which Christians anticipate the second coming of Jesus. Shia Muslims believe both will come on the resurrection day.
"Hugo Chávez was a name known to all nations. His name is reminiscent of pure innocence, kindness, fortitude and love for the people, to serve the people, especially the poor and the victims of colonialism and imperialism by arrogant powers," he wrote. "He is indeed a martyr of the road to service to Venezuelan people, and preserving human and revolutionary values."
Other religious figures in Iran have also echoed Khatami's criticism of Ahmadinejad's remarks about Chávez, one of his closest allies. Hossein Rouhaninejad of Iran's Islamic development organisation said the president's remarks were against Shia Islam beliefs. Another senior cleric, Seyed Mahdi Tabatabaei, chastised Ahmadinejad for "wrong moves", saying his comments were "legally and religiously wrong".
Source: http://www.guardian.co.uk/world/iran-blog/2013/mar/07/ahmadinejad-chavez-resurrected-too-far

Monday, March 4, 2013

Mtazamo wangu--The local church is the hope of the world...!

Mtazamo wangu wa leo...!

Kanisa la mahali pamoja ni tumaini la ulimwengu.Kama kanisa likipoteza tumaini ,linakuwa limepoteza ladha yake na watu hawawezi kufeel kuwepo kanisani.Kanisa haliwezi kuwa community organization.Kanisa sio sehemu ambayo watu wanakuja wakiwa wana magomvi mioyoni mwao. kuwepo kanisani huku watu hata hawasalimiani lakini wananena kwa lugha hadi wanalia.Hali hii inafanya kanisa liwe community organization tu na sio tumaini la ulimwengu unaotuzunguka.Kanisa la mahali pamoja likishindwa kuwafanya watu waishi kwa upendo na amani na kuthaminiana basi tumaini linakuwa limepotea na hapo kanisa linakosa mvuto kwa watu,matokeo yake linakuwa ni community organization ya watu kukutana.Mungu alisaidie kanisa la Tanzania....kwa jina la YESU KRISTO....amen...!