Sunday, September 28, 2008

Breaking news ..ajali morogoro...
Leo hii majira ya saa 9 na nusu ivi nimekutana na ajali mbaya ya basi aina ya costa iliyokuwa inatoka dar kwenda morogoro.Ajali hiyo imetokea maeneo ya karibu na kijijini cha bwawani kilomita chacha kama unaelekea morogoro kutokea kijijini hapo.
Dereva wa gari hiyo alikimbia na utingo wake baada ya ajali hiyo lakini basi tulilokuwa tumepanda tulimlazimisha dereva wetu asimame ili tukawahi kuwapa msaada majeruhi ili wasipoteze maisha na wasiibiwe na vibaka wa maeneo hayo.
Mungu ni mwema hakuna aliyekufa hapo eneo la tukio japo kuna majeruhi kama 5 au 7 hivi ambao hali zao zilikuwa ni mbaya.Na wananchi tuliokuwepo maeneo hayo tuliweza kuwawahisha hospitali ya mkoa ya morogoro.
Tunatakiwa kumwomba Mungu sana kila siku mahali pote na wakati wote maaana tunalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani katika Kristo YESU.

Thursday, September 25, 2008

MAHAKAMA YA KADHI NA OCI..MUNGU AMEANZA KUFANYA KITU..

YALE MAOMBI TULIYOTANGAZA MLIMA SAYUNI YAMEANZA KULETA MATUNDA KABLA HATA KABLA HATUJAANZA KUFUNGA NA KUOMBA KWA AJILI YA JAMBO HILO KAMA TULIVYOTANGAZA MLIMANI SAYUNI WEEK ILIYOPITA..NIMEPATA WADAU WENGI SANA HAPA KENYA AMBAKO NIPO KWA KAMA SIKU 5 HIVI.WADAU WENGI WA MLIMA SAYUNI HAPA NAIROBI AMBAO NI WATANZANIA WAMEONYESHA KUUNGA MKONO MAOMBI HAYA..

SOMA HAPA CHINI HABARI ZA MAASKOFU WA KIPENTEKOSTE

MAASKOFU na wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste (PCT), wamepinga hatua ya serikali kutaka kuingiza Mahakama ya Kadhi katika katiba na nchi kuwa mwanachama wa Umoja wa Nchi za Kiislam (OIC), kwa madai huo ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa PCT, Askofu David Mwasota, alisema kwa miaka mingi Wakristo wa Tanzania wamekuwa wapole, watulivu na wakimya wakiamini kuwa Serikali, Bunge, Mahakama na watu wote waliomo hawategemewi kukiuka katiba.
Alisema waasisi wa nchi hii waliona mbali juu ya suala la amani ya taifa, hivyo wakaweka misingi ya katiba ambayo leo watu wanafurahia matunda yake kwa kuona amani, utulivu na mshikamano na umoja.
“Jambo hili liliwezekana tu pale walipoondoa udini na ukabila ambavyo ndivyo vikwazo vya amani. Kwa mujibu wa katiba, serikali haina dini wala kabila bali watu wake wana dini na makabila.
“Lakini tangu serikali ya awamu ya pili, ya tatu hadi hii ya nne, tumeona kunafanyika juhudi za makusudi kwa baadhi ya viongozi wa serikali, wabunge na viongozi wa dini ya Kiislamu wakijaribu kushinikiza udini kama vile kuitaka kuingiza Mahakama ya Kadhi ndani ya katiba,” alisema askofu huyo.
Aidha, alidai pamoja na wabunge kuwa na haki ya kisheria kubadili katiba, lakini si haki kwao kubadili vipengele ambavyo vinaweza kuhatarisha amani kwa jamii.
Aliongeza kama Wakristo hukumu zao ndogo hufanyika ndani ya dini za Kikristo bila kulazimisha mambo hayo yaingie katika katiba ya nchi, maana kwa kufanya hivyo ni kama kuwalazimisha Watanzania wote kuwa na imani ya Kikristo.
“Kwa kuwa katiba ya nchi hairushusu serikali ya kidini, tunashangazwa ni nini hasa sababu ya Waislamu kulazimisha masuala yao ya imani kuingia na hatimaye kutaka kutambuliwa kinyume na katiba ya nchi na serikali kuendelea kuachilia jambo hili kurudia rudia bungeni inaashiria nini?”alihoji Askofu Mwasota.
Alisema hata kama jambo hili limekubaliwa na chama tawala katika ilani yake, lakini suala hili si la kichama bali ni la kitaifa na halina maslahi kitaifa kwani lina lengo la kugawa Watanzania kidini.
Pia alitahadharisha kuwa endapo bunge litapitisha Mahakama ya Kadhi na kukubali nchi kujiunga na OIC, basi siku hiyo Wakristo nao watataka Bunge lipitishe kipengele cha wakristo kuwa na mahakama yao ndani ya katiba.
Kwa mujibu wa askofu huyo, alisema jambo hilo Wakristo wanalichukulia kama ni la kisiasa zaidi kuliko la kitaifa na kuongeza kuwa wanajua hatari yake kijamii

Tuesday, September 23, 2008

Israel kuongozwa na waziri mkuu mwanamke

Israeli Foreign Minister Tzipi Livni could become Israel's first woman prime minister in 34 years after apparently winning the leadership of the ruling Kadima Party on Wednesday.Livni already is the most powerful woman in the country, having served as foreign minister since 2006. The 50-year old also is Israel's lead negotiator in peace talks with the Palestinians that resumed last November.Livni must form a new coalition within several weeks of Prime Minister Ehud Olmert's resignation, which is expected in the coming days. If Livni succeeds, she will be sworn in as Mr. Olmert's successor. If she fails, she will have to compete in a parliamentary election that polls suggest would be a close contest with Israeli opposition leader Benjamin Netanyahu.Before entering politics, Livni worked for the Mossad, Israel's secret service agency, and practiced law in a private firm for 10 years.Golda Meir served as Israel's first and only woman prime minister to date from 1969 to 1974.Livni was first elected to the Israeli parliament, the Knesset, in 1999 as a member of the right-wing Likud party. She become a cabinet minister in 2001, and held several portfolios in the following years, including the Justice ministry.In November 2005, she joined former Israeli prime minister Ariel Sharon in quitting the Likud party to form the new centrist party, Kadima. Before Sharon fell into a coma in January 2006, he gave Livni the role of foreign minister in his caretaker government.Livni's departure from the Likud marked a significant break with her nationalistic heritage.Her father, Eitan Livni, was a legendary member of the Jewish rebel movement, the Irgun, that fought British troops in Palestine in the 1940s. He was jailed by the British for sabotaging railway lines and other strategic installations.After Israel's War of Independence, Eitan Livni joined the Herut party, a forerunner of the Likud, and served three terms as a Knesset member.

Sunday, September 21, 2008

HOW TO ASK YOUR BOSS FOR A SALARY INCREASE..?

HOW TO ASK YOUR BOSS FOR A SALARY INCREASE..?

One day an employee sends a letter to his boss asking for an increase in his salary!!!

Dear Bo$$

In thi$ life, we all need $ome thing mo$t de$perately. I think you $hould be under$tanding of the need$ of u$
worker$ who have given $o much $upport including $weat and $ervice to your company.

I am $ure you will gue$$ what I mean and re$pond $oon. Your$ $incerely,
Norman $ohThe next day, the employee received this letter of reply:


Dear NOrman,

I kNOw you have been working very hard. NOwadays, NOthing much has changed. You must have NOticed that our company is NOt doing NOticeably well as yet.

NOw the newspaper are saying the world`s leading ecoNOmists are NOt sure if the United States may go into aNOther recession. After
the NOvember presidential elections things may turn bad.

I have NOthing more to add NOw. You kNOw what I mean.

Yours truly,

Manager
Best regards

Friday, September 19, 2008

KUPANDA MLIMA SAYUNI KWA AJILI YA TANZANIA

BWANA YESU ASIFIWE SANA...
WAPENDWA WENGI WAMEKUWA WAKIUNGA MKONO MAOMBI HAYA KWA AJILI YA TANZANIA.

MAOMBI YETU YATAANZA TAREHE 5 MWEZI WA 10 MARA BAADA YA MFUNGO WA MWEZI HUU WA RAMADHANI NA YATADUMU KWA KIPINDI CHOTE CHA BUNGE LA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA.
TUTAWATANGAZIA UTARATIBU MZIMA WA JINSI MAOMBI HAYO YATAKAVYOFANYIKA.
ENDELEA KUTUMA EMAIL YAKO YA KUUNGA MKONO MAOMBI HAYA KWA AJILI YA TANZANIA.

KAMA UNAPENDA KUUNGANA NA WANASAYUNI WENGINE KATIKA KUOMBA KWA AJILI YA HILI...HEBU TUMA EMAIL KWENDA MIWLC@YAHOO.COM na ANDIKA SUBJECT YA EMAIL YAKO "HIVI "KUPANDA MLIMA SAYUNI KWA AJILI YA TANZANIA"KWENYE EMAIL YAKO ANDIKA JINA LAKO KAMILI, UMRI, MAHALI UNAPOISHI KWA SASA,UTAIFA WAKO, JINSIA YAKO,NAMBA YAKO YA SIMU UKIPENDA, PIA ANDIKA KWA KIFUPI KUHUSU KUUNGA KWAKO MKONO MAOMBI HAYA YA MNYORORO...TUTAANZA MAOMBI HAYA KUANZIA TAREHE 05/10/2008 . HIVYO HAKIKISHA UNATUTUMIA EMAIL YAKO KABLA YA TAREHE TAREHE 04/10/2008. N.B: EMAIL ZITAKAZOTUMWA HAPA HATUTAZITANGAZA HAPA UBARIKIWE NA BWANA YESU KRISTO WA NAZARETH.
AMEN

Wednesday, September 17, 2008

KUPANDA MLIMA SAYUNI KWA AJILI YA TANZANIA

Wiki yote hii nimekuwa nikipokea ujumbe mfupi wa simu (sms) kutoka kwa wapendwa mbalimbali unazunguka ili kuiombea Tanzania na bunge letu ili lisipitishe maamuzi haya ya kuiingiza nchi katika umoja wa nchi za kiislamu duniani (OIC) na pia kuliingiza suala la mahakama ya kadhi katika katiba ya nchi.
Jambo hili linaonekana kuwagusa wapendwa wengi na kuchukua hisia za wengi kwani baada ya mfungo wa ramadhani bunge letu litakutana tena Dodoma ili kujadili miswada hii yote au moja kati ya hii.
Swala la msingi hapa kwetu kama watu wa Mungu ni kuiombea nchi yetu.Maombi ni ufunguo wa mambo mengi sana.Hakuna jambo gumu mbele la YESU KRISTO.Biblia inasema vita vyetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka za giza katika ulimwengu wa roho...tukiangusha kila ngome na elimu zipate kumtii KRISTO..maana silaha zetu zina nguvu katika Mungu hata kuangusha ngome.Biblia inaendelea kusema katika Waefeso 6:10 kuwa vaeni silaha zote za MUNGU ili mpate kusimama siku ya uovu..
Sisi mlima sayuni tunaingia kwenye chain prayer (maombi ya mnyororo) kuanzia siku ya leo hadi siku ambayo bunge la jamhuri litakapokaa tena kule dodoma.Tunamwamini Mungu kuwa anajibu maombi...tofauti yetu na wanasiasa ni kuwa sisi hatuwezi kupiga kelele na kuandamana kama wafanyavyo mataifa.ila tumepewa mamlaka ya kufunga na kufungulia mambo hapa duniani na Mungu anafanya pia mbinguni...
Hima watumishi wa Mungu aliye hai...tusimame katika zamu zetu na kuanza sasa kwa bidii kuiombea nchi..
KAMA UNAPENDA KUUNGANA NA WANASAYUNI WENGINE KATIKA KUOMBA KWA AJILI YA HILI...HEBU TUMA EMAIL KWENDA MIWLC@YAHOO.COM na ANDIKA SUBJECT YA EMAIL YAKO "HIVI "KUPANDA MLIMA SAYUNI KWA AJILI YA TANZANIA"
KWENYE EMAIL YAKO ANDIKA JINA LAKO KAMILI, UMRI, MAHALI UNAPOISHI KWA SASA,UTAIFA WAKO, JINSIA YAKO,NAMBA YAKO YA SIMU UKIPENDA, PIA ANDIKA KWA KIFUPI KUHUSU KUUNGA KWAKO MKONO MAOMBI HAYA YA MNYORORO...TUTAANZA MAOMBI HAYA KUANZIA TAREHE 05/10/2008 . HIVYO HAKIKISHA UNATUTUMIA EMAIL YAKO KABLA YA TAREHE TAREHE 04/10/2008.
N.B: EMAIL ZITAKAZOTUMWA HAPA HATUTAZITANGAZA HAPA

UBARIKIWE NA BWANA YESU KRISTO WA NAZARETH.
AMEN

Saturday, September 13, 2008

Mama wawili kuingiza sokoni albam ya injili

Muimbaji wa injili wa siku nyingi anayejulikana kwa jina la mama wawili ameuambia mlima sayuni kuwa anatarajia kuingiza sokoni albam yake ya kwanza ya injili siku si nyingi.
Pichani anaonekana akirekodi mkanda wa video wa moja kati ya nyimbo zilizoko katika albam hiyo katika kanisa la Faith Word Church Mnazi Mmoja kwa Pastor Andew.True Friendship at all the time


mtade (Baba Chinyemi) akiwa na Marco Salimu (Baba Angel)...unaweza kuwaona zaidi katika www.digitalbraintz.com

Mary Munga--born-again herbalist

Mrs Mary Auma Munga, a 50year-old primary school teacher from the Siaya district in Kenya, is a herbalist with a difference. For 24 years she has been practising herbal medicine, but since she became a born-again Christian, she now does it for the glory of God. And she treats her patients free.
Mary Munga also has a special gift. She says she can tell her patients' problems before they tell her what is wrong. She says that the moment a patient comes to her, no matter what the ailment, she begins to suffer the patient's pains. They are amazed at her total understanding of their illnesses. She says it comes to her in a vision, which also gives her an insight into the cure and what type of herbs to prescribe.
Munga inherited her trade from her ancestors. For two decades she practised traditional medicine like other native herbalists, making sacrifices to dead ancestors.
But one day when her son was very sick, suffering from a strange skin disease, she says God came to her in a vision and told her of the right kind of herb to use to cure her son.
She picked the leaves of the guarva herb, boiled them and gave them to her son to drink. The boy's skin rash disappeared and has never recurred since.
"One day I was asleep when God came to me in a vision. He told me that treating people with herbs was not sinful," Mary told Palaver, "what was sinful was to do the treatment in the name of dead ancestors."
So Mary became a born-again Christian and now carries out all her treatments in the name of God. She says that before her conversion she was a traditional herbalist charging people for their cure. Now she makes the same treatments but charges no fee.
"God gave me the talent free of charge, so I now help God's children free of charge," said Mary. She says it is God who now guides her in all her cases giving her an understanding of the illness and telling her the right herbs to use for a cure.
The Kisumu based Gender Centre has recently sponsored her to conduct more research into various plants in the Siaya district. Working under Mrs Asenath Bole Odaga, the head of the Gender Centre, she is compiling a list of all the herbs she uses and what illnesses they treat.
She has also begun farming on a single acre plot to grow various herbs plus cocoa, milo, soya beans, carrots, yams, groundnuts, and traditional greens such as mito and osuga. Much of her crops are used to make special health giving beverages from milo, cocoa and soya beans prepared in novel ways. These drinks are much appreciated in local schools and her beverages are giving her a profitable business. This has given her some capital so that she can afford to care for 14 orphan children, whose parents have died of AIDS-related diseases.
Mary has no cure for AIDS but she thinks much can be done through education and creating awareness of its dangers to the public at large.

Tiba ya mitishamba kwa watu waliokoka ni kibiblia?

Week hii nimekutana na challenge nyingi sana kuhusu tiba za mitishamba kwa watu waliokoka..
Je..ni salama na ni kibiblia au ni kinyume na Biblia takatifu?
Kuna mtu akaniuliza kama nyumbani kwake amepanda mti wa muarobaini na akienda kuchuma majani yake na kujitibu malaria au ugonjwa wowote je hiyo ni dhambi? je kuna tofauti gani na tabibu anayetumia mitishamba kutibu watu na akiwa ameokoka?
Najua kuna majibu tofauti kuhusu hili ila naomba majibu yote yatoke katika maandiko matakatifu au yawe na support ya maandika matakatifu..

Tuesday, September 9, 2008

God's Delays Are Not Denials


God answers prayer, but not always our way. He is rarely rushed or in a hurry, as is evident in His Creation: It takes Him time to make a baby, a flower, a tree, a sunset--or even a blade of grass. You can't rush God. You've got to wait till it's God's time. Sometimes God delays answering prayer until you have learned the lesson He is trying to teach you. Or perhaps He is waiting for the circumstances to be ready for the result that He wants to bring. Take for example the man in the Bible who was blind from birth: He had had to be blind all his life, so that everybody would know it, & so that when Jesus came along one day & marvelously healed him, God would be glorified. (See John 9.) It may sometimes take years before you know why God didn't answer prayer as you thought He should, or right when you asked Him to, but the time will come, & you'll know God was right! Wait on the Lord!The greatest darkness is just before dawn, the greatest desperation is just before Salvation! The greatest hopelessness attacks just before rescue! So never doubt for a moment that God is going to answer--And He will! Trust Him & thank Him for the answer--even if you don't see it immediately! You'll be glad you trusted Him tomorrow!

"Fret Not Thyself For Tomorrow"

"Fret Not Thyself For Tomorrow"
It's always tomorrow that we are tempted to worry about. But God's Word forbids fear over the future. Jesus said, "Take no thought for the morrow: For the morrow shall take thought for the things of itself." The future will take care of itself! "For sufficient unto the day (today) is the evil thereof." (Mat.6:34) That is God's warning, commandment & promise!You are to enjoy today & take things as they come & let tomorrow take care of itself! "For as thy days, so shall thy strength be!" (Deu.33:25) God will give you power for the hour, grace for the trial--AT the hour & when it comes.--Not before! "He Who hath begun a good work in you is going to perfect it unto the end! For He is the Author & the Finisher of our faith; Who hath delivered, Who doth deliver, & Who will yet deliver!" (Phi.1:6; Heb.12:2; 2Cor.1:10) He loves you & cares for you & is going to take care of you no matter what.So for God's sake, don't worry about tomorrow! That's not your concern, that's not your worry, that's none of your business! That's God's business!"Oh, I've nothing to do with tomorrow!My Savior will make that His care.Its grace & its strength I can't borrow,So why should I borrow its care?"Trust in the Lord!--Amen?

Friday, September 5, 2008

"Joy In The Presence Of The Angels Of God"

"Joy In The Presence Of The Angels Of God"
Each time a new soul is born into the Kingdom of God, it's almost like the birth of a child. Although the baby is delivered sometimes in pain, afterward the pain is forgotten in the delight of a new soul born into this World!--And the same joy, only greater, is experienced at the birth of a new spirit into the Kingdom of God! One saved soul makes all Heaven rejoice, & is certainly sufficient payment for all the hard work & sacrifices & a few little hard trials & tribulations that we may go through.All Heaven rejoices & all the Angels rejoice more over one lost sheep that's found, each soul saved, than over all the ninety-&-nine & all the rest who are already saved & rescued! (Lk.15:7)If the Angels of Heaven rejoice over every soul that's saved, they certainly must also rejoice over our obedience to God & our service for the Lord! When your time of reward & recognition comes, are the Heavens & the Angels of God going to jump for joy over your faithfulness & your diligent service for the Lord & your sacrificial giving?

Wednesday, September 3, 2008

Pastor Joseph Justine

HADI TUNAANDIKA HAPA MSIBA WA PASTOR JOSEPH JUSTINE WA TAYOMI NA CASFETA UMEHAMISHIWA KIJIJINI KWAKE MELELA NJE YA MJI WA MOROGORO NA ANAZIKWA JIONI HII YA LEO HUKO HUKO.
ASUBUHI YA LEO WATU MBALIMBALI WALIHUDHURIA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU PALE KINONDONI DPC WALIONA JINSI UMATI WA WATU WENGI WALIVYOJITOKEZA NA KUJAWA NA SIMANZI HUKU WENGINE WAKIJIULIZA MASWALI MENGI BILA MAJIBU WA MUHSTAKABARI MZIMA WA HUDUMA YA TAYOMI AMBAYO KWA KIASI KIKUBWA IMEKUWA IKISIMAMIWA NA KUENDESHWA CHINI YA MAONO YA MTUMISHI HUYO WA MUNGU.
WATU WENGI WAKIWEMO WATUMISHI WENGI WAKUBWA NA WANAFUNZI WA VYUO,SEKONDARI NA SHULE ZA MSINGI NA HATA WALE WALIOMALIZA VYUO NA MASHULE WALIKUWEPO KUSHUHUDIA IBADA HIYO ILIYOJAA SIMANZI NA KUONYESHA JINSI AMBAVYO MCHUNGAJI JOSEPH JUSTINE ALIKUWA NI MTU WA WATU.
MLIMA SAYUNI UNAIPONGEZA KAMATI YA MAANDALIZI KWA KUJITOLEA MUDA WAO NA FEDHA, BILA KUWASAHU WALE WOTE WALIOJITOKEZA KUHUDHURIA MAZISHI HAYO KWA NJIA YA KUTUTUMIA SMS NA HATA KUFIKA PHYSICALLY.

Tuesday, September 2, 2008

BREAKING NEWS

HABARI ZILIZOTUFIKIA DAWATI LETU LA HABARI HAPA MLIMA SAYUNI ZIMETUSHTUA SANA. MCHUNGAJI WA VIJANA NA MWENYE WITO NA UTUMISHI KWA VIJANA NA WANAFUNZI HAPA TANZANIA,REV.JOSEPH JUSTINE HATUNAYE TENA KWANI AMETANGULIA KWA BWANA JANA MAJIRA YA SAA MOJA USIKU KATIKA HOSPITALI YA AGHA KHAN JIJINI DAR ES SALAAM. MCHUNGAJI JUSTINE AMBAYE ALIKUWA NI MKURUGENZI MKUU WA HUDUMA YA TAYOMI HAPA NCHINI ALIKUWA AKIUGUA KWA ZAIDI YA MWEZI MMOJA SASA NA AMEKUWA AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA HINDU MANDALI NA AGHA KHAN ZOTE ZA JIJINI. MWILI WA MAREHEMU UTAAGWA RASMI KESHO ASUBUHI SAA 1 NA NUSU PALE KATIKA KANISA LA KINONDONI DPC NA BAADAYE KUSAFIRISHWA KUPELEKWA MOROGORO KIJIJINI KWAKE MELELA NJE KIDOGO YA MANISPAA YA MOROGORO.ATAZIKWA KIJIJINI KWAKE KESHO MIDA YA MCHANA.USAFIRI KWA YEYOTE ATAKAYEPENDA KWENDA UTAKUWEPO. MLIMA SAYUNI UNAUNGANA NA WANAFUNZI,VIJANA NA WANACASFETA WOTE NCHINI NA WALE WALIO NJE YA NCHI,ZAIDI SANA NA FAMILIA YA MAREHEMU NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA HUU.MAREHEMU AMEACHA MKE NA WATOTO WANNE.TUTAENDELEA KUWAPATIENI HABARI ZAIDI KADRI TUTAKAVYOSIKIA KUHUSIANA NA MSIBA HUU. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE. AMEN