Wednesday, September 17, 2008

KUPANDA MLIMA SAYUNI KWA AJILI YA TANZANIA

Wiki yote hii nimekuwa nikipokea ujumbe mfupi wa simu (sms) kutoka kwa wapendwa mbalimbali unazunguka ili kuiombea Tanzania na bunge letu ili lisipitishe maamuzi haya ya kuiingiza nchi katika umoja wa nchi za kiislamu duniani (OIC) na pia kuliingiza suala la mahakama ya kadhi katika katiba ya nchi.
Jambo hili linaonekana kuwagusa wapendwa wengi na kuchukua hisia za wengi kwani baada ya mfungo wa ramadhani bunge letu litakutana tena Dodoma ili kujadili miswada hii yote au moja kati ya hii.
Swala la msingi hapa kwetu kama watu wa Mungu ni kuiombea nchi yetu.Maombi ni ufunguo wa mambo mengi sana.Hakuna jambo gumu mbele la YESU KRISTO.Biblia inasema vita vyetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka za giza katika ulimwengu wa roho...tukiangusha kila ngome na elimu zipate kumtii KRISTO..maana silaha zetu zina nguvu katika Mungu hata kuangusha ngome.Biblia inaendelea kusema katika Waefeso 6:10 kuwa vaeni silaha zote za MUNGU ili mpate kusimama siku ya uovu..
Sisi mlima sayuni tunaingia kwenye chain prayer (maombi ya mnyororo) kuanzia siku ya leo hadi siku ambayo bunge la jamhuri litakapokaa tena kule dodoma.Tunamwamini Mungu kuwa anajibu maombi...tofauti yetu na wanasiasa ni kuwa sisi hatuwezi kupiga kelele na kuandamana kama wafanyavyo mataifa.ila tumepewa mamlaka ya kufunga na kufungulia mambo hapa duniani na Mungu anafanya pia mbinguni...
Hima watumishi wa Mungu aliye hai...tusimame katika zamu zetu na kuanza sasa kwa bidii kuiombea nchi..
KAMA UNAPENDA KUUNGANA NA WANASAYUNI WENGINE KATIKA KUOMBA KWA AJILI YA HILI...HEBU TUMA EMAIL KWENDA MIWLC@YAHOO.COM na ANDIKA SUBJECT YA EMAIL YAKO "HIVI "KUPANDA MLIMA SAYUNI KWA AJILI YA TANZANIA"
KWENYE EMAIL YAKO ANDIKA JINA LAKO KAMILI, UMRI, MAHALI UNAPOISHI KWA SASA,UTAIFA WAKO, JINSIA YAKO,NAMBA YAKO YA SIMU UKIPENDA, PIA ANDIKA KWA KIFUPI KUHUSU KUUNGA KWAKO MKONO MAOMBI HAYA YA MNYORORO...TUTAANZA MAOMBI HAYA KUANZIA TAREHE 05/10/2008 . HIVYO HAKIKISHA UNATUTUMIA EMAIL YAKO KABLA YA TAREHE TAREHE 04/10/2008.
N.B: EMAIL ZITAKAZOTUMWA HAPA HATUTAZITANGAZA HAPA

UBARIKIWE NA BWANA YESU KRISTO WA NAZARETH.
AMEN

No comments: