Wednesday, September 3, 2008

Pastor Joseph Justine

HADI TUNAANDIKA HAPA MSIBA WA PASTOR JOSEPH JUSTINE WA TAYOMI NA CASFETA UMEHAMISHIWA KIJIJINI KWAKE MELELA NJE YA MJI WA MOROGORO NA ANAZIKWA JIONI HII YA LEO HUKO HUKO.
ASUBUHI YA LEO WATU MBALIMBALI WALIHUDHURIA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU PALE KINONDONI DPC WALIONA JINSI UMATI WA WATU WENGI WALIVYOJITOKEZA NA KUJAWA NA SIMANZI HUKU WENGINE WAKIJIULIZA MASWALI MENGI BILA MAJIBU WA MUHSTAKABARI MZIMA WA HUDUMA YA TAYOMI AMBAYO KWA KIASI KIKUBWA IMEKUWA IKISIMAMIWA NA KUENDESHWA CHINI YA MAONO YA MTUMISHI HUYO WA MUNGU.
WATU WENGI WAKIWEMO WATUMISHI WENGI WAKUBWA NA WANAFUNZI WA VYUO,SEKONDARI NA SHULE ZA MSINGI NA HATA WALE WALIOMALIZA VYUO NA MASHULE WALIKUWEPO KUSHUHUDIA IBADA HIYO ILIYOJAA SIMANZI NA KUONYESHA JINSI AMBAVYO MCHUNGAJI JOSEPH JUSTINE ALIKUWA NI MTU WA WATU.
MLIMA SAYUNI UNAIPONGEZA KAMATI YA MAANDALIZI KWA KUJITOLEA MUDA WAO NA FEDHA, BILA KUWASAHU WALE WOTE WALIOJITOKEZA KUHUDHURIA MAZISHI HAYO KWA NJIA YA KUTUTUMIA SMS NA HATA KUFIKA PHYSICALLY.

1 comment:

Mary Damian said...

Mungu na awape faraja!