Thursday, September 25, 2008

MAHAKAMA YA KADHI NA OCI..MUNGU AMEANZA KUFANYA KITU..

YALE MAOMBI TULIYOTANGAZA MLIMA SAYUNI YAMEANZA KULETA MATUNDA KABLA HATA KABLA HATUJAANZA KUFUNGA NA KUOMBA KWA AJILI YA JAMBO HILO KAMA TULIVYOTANGAZA MLIMANI SAYUNI WEEK ILIYOPITA..NIMEPATA WADAU WENGI SANA HAPA KENYA AMBAKO NIPO KWA KAMA SIKU 5 HIVI.WADAU WENGI WA MLIMA SAYUNI HAPA NAIROBI AMBAO NI WATANZANIA WAMEONYESHA KUUNGA MKONO MAOMBI HAYA..

SOMA HAPA CHINI HABARI ZA MAASKOFU WA KIPENTEKOSTE

MAASKOFU na wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste (PCT), wamepinga hatua ya serikali kutaka kuingiza Mahakama ya Kadhi katika katiba na nchi kuwa mwanachama wa Umoja wa Nchi za Kiislam (OIC), kwa madai huo ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa PCT, Askofu David Mwasota, alisema kwa miaka mingi Wakristo wa Tanzania wamekuwa wapole, watulivu na wakimya wakiamini kuwa Serikali, Bunge, Mahakama na watu wote waliomo hawategemewi kukiuka katiba.
Alisema waasisi wa nchi hii waliona mbali juu ya suala la amani ya taifa, hivyo wakaweka misingi ya katiba ambayo leo watu wanafurahia matunda yake kwa kuona amani, utulivu na mshikamano na umoja.
“Jambo hili liliwezekana tu pale walipoondoa udini na ukabila ambavyo ndivyo vikwazo vya amani. Kwa mujibu wa katiba, serikali haina dini wala kabila bali watu wake wana dini na makabila.
“Lakini tangu serikali ya awamu ya pili, ya tatu hadi hii ya nne, tumeona kunafanyika juhudi za makusudi kwa baadhi ya viongozi wa serikali, wabunge na viongozi wa dini ya Kiislamu wakijaribu kushinikiza udini kama vile kuitaka kuingiza Mahakama ya Kadhi ndani ya katiba,” alisema askofu huyo.
Aidha, alidai pamoja na wabunge kuwa na haki ya kisheria kubadili katiba, lakini si haki kwao kubadili vipengele ambavyo vinaweza kuhatarisha amani kwa jamii.
Aliongeza kama Wakristo hukumu zao ndogo hufanyika ndani ya dini za Kikristo bila kulazimisha mambo hayo yaingie katika katiba ya nchi, maana kwa kufanya hivyo ni kama kuwalazimisha Watanzania wote kuwa na imani ya Kikristo.
“Kwa kuwa katiba ya nchi hairushusu serikali ya kidini, tunashangazwa ni nini hasa sababu ya Waislamu kulazimisha masuala yao ya imani kuingia na hatimaye kutaka kutambuliwa kinyume na katiba ya nchi na serikali kuendelea kuachilia jambo hili kurudia rudia bungeni inaashiria nini?”alihoji Askofu Mwasota.
Alisema hata kama jambo hili limekubaliwa na chama tawala katika ilani yake, lakini suala hili si la kichama bali ni la kitaifa na halina maslahi kitaifa kwani lina lengo la kugawa Watanzania kidini.
Pia alitahadharisha kuwa endapo bunge litapitisha Mahakama ya Kadhi na kukubali nchi kujiunga na OIC, basi siku hiyo Wakristo nao watataka Bunge lipitishe kipengele cha wakristo kuwa na mahakama yao ndani ya katiba.
Kwa mujibu wa askofu huyo, alisema jambo hilo Wakristo wanalichukulia kama ni la kisiasa zaidi kuliko la kitaifa na kuongeza kuwa wanajua hatari yake kijamii

No comments: