Friday, December 14, 2007

Is Prophet T.B Joshua controversial ?

Anaitwa Bishop T.B Joshua, anajulikana sana Nigeria kwa huduma yake ya uponyaji na kutenda miujiza mikubwa isiyo ya kawaida.Tembelea tovuti take utaona zaidi.


Ila huko kwao Nigeria kuna baadhi wanampinga na wengine wanamuunga mkono.Wanaompinga wanamtuhumu kwa kuponya kwa nguvu za uchawi.Na wengine wanamuunga mkono wakisema ni mtumishi wa Mungu.Mwenye anajiita "a man in the Synagogue"


Nenda kweny forum hii uone malumbano ya wanigeria kumuhusu.


7 comments:

Anonymous said...

I am not surprised that cant get this around their little minds, because biblia katika 1wakorintho 2:14 inaweka wazi “…mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu, maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulika kwa jinsi ya Rohoni”
Wanayoyasema kuhusu T. B. Joshua si mageni, the same thing happened to Jesus, aliambiwa na mafarisayo na wajinga wengine ana belizebuli,na anafanya miujiza kwa nguvu za giza. this is a product of corrupted minds of people, ambao mungu wao ni mdoogo sana hata asiweze kufanya miujiza ya jinsi atendavyo prophet T. B. Joshua. Yesu alishasema, aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo atazifanya, naam na kubwa kuliko hizo atafanya maana mimi nakwenda kwa baba. Thats what TB joshua is doing, the same thing that peter and others did, ie Preaching the word of God and demonstrating it wit Signs and Wonders. He is a man of God. wakati wa injili ya maneno matupu umekwisha, kama neno linasema katika Mathayo 8:17
.............Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukua magonjwa yetu" we expect to see sick people delivered by the name of Jesus and walking free, si biashara ya kuambiwa vumilia tu, duniani mna dhiki nyingi.... Injili ya maneno matupu imetosha, we need to see God at work because watu wa mungu wanateseka sana na uonevu wa shetani.

Anonymous said...

Jamani, mi nahisi tunajaribu kutoa majibu rahis kwa maswali magumu. Tujiulize wakati mambo hayo yoote yanapotendeka je utukufu anapewa nani?
Je sisi tunaotumiwa tunakuwa na maoni gani kuhusu hizo huduma zetu?

Maana biblia inasema "...walakini msiyahukumu mawazo yake" Rumi 14. Sasa kama hatujayajua mawazo yake hatuwezi kuonywa tusiyahukumu na hatuwezi kuyajua mawazo yake mpaka ama ameyatenda au kuyasema, so tuangalie sana jinsi wanavyotenda na kusema kabla hatujawakubali ama kuwakataa hawa watumishi kwa vile kuna pia wale watakaosema "...Bwana, tulitoa pepo kwa jila lako, na kwa jina lako......na kutenda isahara nyingi...." na bado hatakuwa hawajui.

melckzedek D. mbise said...

jamani watumishi wasimseme mtumishi wa Mungu TB Joshua ila wanatakiwa kujiuliza anawezaje kutumiwa na Mungu kiasi hicho. kwa kifupi TB Joshua alifunga siku arobaini ndiyo akapata nguvu za Mungu kufanya miujiza hiyo. Sasa watumishi wa Mungu wa siku hizi hawapendi maombi wanafanya maombi ya kubeep na wanategemea kuona miujiza wasipoona miujiza wanaconclude kwamba miujiza haipo siku hizi na kuwaona wanaotumiwa na Mungu kutenda miujiza kuwa wanatumia uchawi. Hivyo me nafikiri watumishi wa Mungu wafunge na kuomba watamwona Mungu sasa wewe unakula tu na unategemea kuona miujiza ya Mungu hiyo haiwezekani you have to seek God diligently. Tangu enzi za Yohana mbatizaji ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu na wenye nguvu wameuteka na hao wasiitwe wachawi hiyo ni imani potofu na haba be blessed!!!

Paschal said...

Tatizo hao wapingao ni wanadamu hata wasiojishughulisha na Mungu lakini wanaamini kuwa Mungu yupo.wamekosa uchaji wa Mungu ndio maana wanabaki kushangaa shetani kashika ufahamu wao.wenye macho,hawaoni.masikio wanayo,hawasikii.Tatizo hao wapingao ni wanadamu hata wasiojishughulisha na Mungu lakini wanaamini kuwa Mungu yupo.wamekosa uchaji wa Mungu ndio maana wanabaki kushangaa shetani kashika ufahamu wao.wenye macho,hawaoni.masikio wanayo,hawasikii.

Anonymous said...

Wanaompinga sio wasio mjua Mungu tu,kwa taarifa wanaompinga zaidi ni watumishi wenzake,Umoja wa makanisa ya KIPENTECOSTE NIGERIA wamekataa kuitambua huduma yake,na wana madai yao na hoja zao,ni vizuri kujua na upande huo wana mpinga kwa lipi.

Anonymous said...

Mwacheni Mungu aitwe Mungu,wanaotumika waachwe watumike ili Mungu wetu apate utukufu anaostahili.kwa kuwa walioshindwa wana maneno mengi na hofu za kijinga.

Anonymous said...

How come kumjadili mtumishi wa mwingine. je ninani aliyewatuma kumjadili na hao wanaomkubali au kumkataa je ni kweli Mungu amewatuma kuuelezea uma au wanapoteza muda kwa sababu hawana cha kufanya.
Ushauri: MTAFUTENI MUNGU JINYENYEKESHENI MBELE ZAKE MUNGU, ACHENI. MUNGU AKIKUTUMA IS FINE LAKINI ACHENI UBABAISHAJI MPENI MUNGU UTUKUFU KWA YALE MAZURI YANAYOTENDEKA.