Wednesday, November 17, 2010

Mwanamke akutwa uchi kanisani


Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35 mpaka 40 (pichani), amekutwa ndani ya Kanisa la House of Prayer Center ‘HPC’ akiwa mtupu hali iliyomchanganya akili Mchungaji wa kanisa hilo.

Tukio hilo la aina yake lilijiri saa kumi ya alfajiri katikati ya wiki iliyopita, Tabata ya Liwiti jijini Dar es Salaam.

Mashuhuda wa mkasa huo walilitonya Risasi Mchanganyiko kuwa, mwanamke huyo alitambulika kwa jina la Neema Komba na alikuwa na binti yake wa miaka 3 ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

Mashuhuda hao waliendelea kusema kwamba, katika kujieleza kwake, mama huyo alisema ni mwenyeji wa mkoa wa Ruvuma, akitokea Wilaya ya Songea, alifika jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusalimia ndugu na jamaa.

Aidha, taarifa kutoka katika kanisa hilo zinasema kuwa, Neema alinaswa na walinzi wa kanisa hilo kitu ambacho kilizua hofu na tafrani kanisani hapo kwa muda wa saa kadhaa.

“Ile hali ilizua hofu na tafrani kubwa kwa muda wa saa kadhaa, unajua mambo kama haya halafu kwa kanisani ni vitu vya ajabu sana,” alisema muumini mmoja wa kanisa hilo.

Aliongeza kuwa, ilikuwa walinzi wa kanisa hilo wanafanya doria kwa kuzunguka kila eneo la kanisa hilo, ndipo waliposikia sauti ya nyao za miguu ya binadamu, “ndipo walipoamua kuingia na kumkuta mama huyo akiwa uchi jambo ambalo lilitushangaza sana ukilinganisha na muda wenyewe,” aliongeza muumini huyo.

Inadaiwa baada ya hapo walinzi hao walimjulisha Mchungaji wa kanisa hilo kwa lengo la kumtambua mwanamke huyo lakini naye alionekana kuwa mgeni machoni pake.

Hata hivyo, baadhi ya watu walionesha masikitiko yao kwa hali ya mama huyo, ingawa baadhi yao waliamini ni mchawi na kutaka kumpa kichapo cha mbwa mwizi.

Mwishowe, uongozi wa kanisa hilo ukiongozwa na Mchungaji Patrick Kayimbi Emanuel na akina mama waliokuwepo eneo la tukio walijitolea kumpa khanga kwa nia ya kujisitiri.

Akihojiwa na Mchungaji Kayimbi, mwanamke huyo alisema hajui amefikaje ndani ya kanisa hilo kwani ana akili zake timamu.

Baadaye Mchungaji Kayimbi alitia neneo la Bwana kwa nia ya kufukuza mapepo akiamini ndiyo yaliyomfikisha mwanamke huyo ndani ya kanisa hilo.

Lakini wakati hayo yakiendelea walitokea ndugu zake waliodai ndiyo wenyeji wa mwanamke huyo, Dar na kuuomba uongozi wa kanisa hilo kumwachia ndugu yao waende naye nyumbani.

Mchungaji aliwakubalia lakini kwa masharti kuwa, siku iliyofuata wamrudishe kwa ajili ya kuendelea kumfanyia maombi kupitia Neno la Mungu.

Naye Mchungaji huyo alipoulizwa na Risasi kuhusiana na hali hiyo huku akionekana kushangaa, alisema kabla ya tukio hilo kutokea walifanya maombi kwa muda wa siku tatu mfululizo ili kuombea yale yote mabaya ambayo yanaweza kutokea kanisani hapo, kasema: “Naamini kuwa matokeo yake ndiyo haya sasa.”

Source: Globalpublisherstz.info

1 comment:

Anonymous said...

Pengine haikutakiwa kuweka picha yake. Natumaini kusuduio la habari hii si kumtangaza wala kumdharirisha mama huyo picha.

Kwani nguvu za Mungu zitampanya na kumfanya awe mtumishi na chombo kizuri kwa ajiri ya Utukufu wa Bwana