Wednesday, November 17, 2010

Kazi ya Mungu


Kayala na mkewe wakimwabudu Mungu wakati wa ibada ya kuabudu.

MHARIRI Msaidizi wa gazeti la Risasi, George Kayala, pamoja na mkewe, Kabula J. George, ambaye ni muimbaji wa muziki wa Injili nchini wamehitimu masomo ya uchungaji katika Chuo cha Uchungaji na Unabii kilichopo jijini Dar es Salaam na mahafali yao kufanyika Novemba 13, 2010 ndani ya Ukumbi wa Huduma ya Neno la Upatanisho iliyopo Bustani ya Edeni (Matembele ya Kwanza) iliyopo Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Siku ya mahafali hayo, Kayala alipewa zawadi ya kufanya vizuri katika masomo ya kitumishi kwa kushika nafasi ya pili kati ya wahitimu 25.


Kayala na mkewe wakimchezea Mungu wakati wa ibada ya kusifu.


Kabula J.George akimwabudu Mungu siku ya mahafali.


Kabula akimsifu Mungu kabla ya kupakwa mafuta ya kuwa watumishi.


Kayala na mkewe (kulia) wakimwimbia Mungu pamoja na mwimbaji mwenzao kutoka Moshi, Renata Samba.Kayala akiwa katika pozi baada ya kupewa zawadi ya kufanya vizuri darasani.


Source: globalpublisherstz.info


No comments: