ULE usemi wa wahenga kuwa Nabii hathaminiwi kwao ulitimia hivi karibuni baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Felloship, Zachary Kakobe kuwaliza maelfu ya Wazambia kutokana na kuwaombea na kufanikiwa kupona magonjwa mbalimbali.
Katika mikutano yake ambayo aliifanya kwa siku tano mfululizo kwenye kiwanja kikubwa na ndani ya makanisa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa ya Lusaka iliyopewa jina la Lusaka Great Miracle Crusade, wagonjwa mbalimbali waliletwa ambapo Askofu Kakobe aliwaombea wakapona.
Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa nchini Zambia, Mchungaji Boniface Nkande alisema pamoja na kwamba wahubiri mbalimbali wa kimataifa hufika nchini humo, mikutano ya Askofu Kakobe imehudhuriwa na umati mkubwa wa watu ambao haujawahi kutokea.
Aidha, Rais Mstaafu wa Zambia, Frederick Chiluba na mkewe walivutiwa na kupagawa na maajabu aliyoyafanya Askofu Kakobe kutokana na maombi yake kwa wagonjwa na katika nchi yake na akaamua kumualika nyumbani kwake ambapo mchungaji huyo wa roho za watu alikwenda na kuibariki nchi ya Zambia.
Source: Globalpublisherstz.info
No comments:
Post a Comment