Tuesday, September 2, 2008

BREAKING NEWS

HABARI ZILIZOTUFIKIA DAWATI LETU LA HABARI HAPA MLIMA SAYUNI ZIMETUSHTUA SANA. MCHUNGAJI WA VIJANA NA MWENYE WITO NA UTUMISHI KWA VIJANA NA WANAFUNZI HAPA TANZANIA,REV.JOSEPH JUSTINE HATUNAYE TENA KWANI AMETANGULIA KWA BWANA JANA MAJIRA YA SAA MOJA USIKU KATIKA HOSPITALI YA AGHA KHAN JIJINI DAR ES SALAAM. MCHUNGAJI JUSTINE AMBAYE ALIKUWA NI MKURUGENZI MKUU WA HUDUMA YA TAYOMI HAPA NCHINI ALIKUWA AKIUGUA KWA ZAIDI YA MWEZI MMOJA SASA NA AMEKUWA AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA HINDU MANDALI NA AGHA KHAN ZOTE ZA JIJINI. MWILI WA MAREHEMU UTAAGWA RASMI KESHO ASUBUHI SAA 1 NA NUSU PALE KATIKA KANISA LA KINONDONI DPC NA BAADAYE KUSAFIRISHWA KUPELEKWA MOROGORO KIJIJINI KWAKE MELELA NJE KIDOGO YA MANISPAA YA MOROGORO.ATAZIKWA KIJIJINI KWAKE KESHO MIDA YA MCHANA.USAFIRI KWA YEYOTE ATAKAYEPENDA KWENDA UTAKUWEPO. MLIMA SAYUNI UNAUNGANA NA WANAFUNZI,VIJANA NA WANACASFETA WOTE NCHINI NA WALE WALIO NJE YA NCHI,ZAIDI SANA NA FAMILIA YA MAREHEMU NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA HUU.MAREHEMU AMEACHA MKE NA WATOTO WANNE.TUTAENDELEA KUWAPATIENI HABARI ZAIDI KADRI TUTAKAVYOSIKIA KUHUSIANA NA MSIBA HUU. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE. AMEN

1 comment:

Anonymous said...

ooh My god, bwana ampumzishe kwa aman

pia mimi naomba msaada wenu wapendwa, BWANA YESU ASIWE WAPENDWA,, MIMI NAITWA IRENE JOSEPH, NINASOMA HAPA UK,, NINAMTAFUTA ANGELA LUBALLA ALIYERUDISHA TAJI LA REDDS, KUNA KITU NATAKA KUONGEA NAYE, naomba kama angela ukisoma hii, au rafiki yeyote wa angela tuwasiliane kwa kutumia email hii irene20002000@yahoo.com,, kama una email yake au namba yake ya simu nitafurahi na kumshukuru yeyete atakayeniunganisha naye
Mungu awabariki sana