Sunday, September 28, 2008

Breaking news ..ajali morogoro...








Leo hii majira ya saa 9 na nusu ivi nimekutana na ajali mbaya ya basi aina ya costa iliyokuwa inatoka dar kwenda morogoro.Ajali hiyo imetokea maeneo ya karibu na kijijini cha bwawani kilomita chacha kama unaelekea morogoro kutokea kijijini hapo.
Dereva wa gari hiyo alikimbia na utingo wake baada ya ajali hiyo lakini basi tulilokuwa tumepanda tulimlazimisha dereva wetu asimame ili tukawahi kuwapa msaada majeruhi ili wasipoteze maisha na wasiibiwe na vibaka wa maeneo hayo.
Mungu ni mwema hakuna aliyekufa hapo eneo la tukio japo kuna majeruhi kama 5 au 7 hivi ambao hali zao zilikuwa ni mbaya.Na wananchi tuliokuwepo maeneo hayo tuliweza kuwawahisha hospitali ya mkoa ya morogoro.
Tunatakiwa kumwomba Mungu sana kila siku mahali pote na wakati wote maaana tunalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani katika Kristo YESU.

No comments: