Kongoma kubwa la wajasiliamali lililoandaliwa na kampuni inayokua kwa kasi sana hapa nchini ya DigitalBrain lilifana sana siku ya jumamosi tarehe 6/6/2009.
Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa Mbinga mashariki -CCM Mheshimiwa Gaudency Kayombo, alisema kuwa amefurahishwa sana na hatua iliyochukuliwa na DigitalBrain ya kuwaleta wajasiliamali kwa pamoja na kuwafundisha masomo hayo ambayo yanalenga katika kuwakomboa watanzania na wimbi la umaskini.
Katika kongomano hilo ambalo wajasiliamali takribani ya 120 walihudhuria na kupewa mafunzo ya kina kabisa jinsi ya kufanikiwa kibiashara na kubadirishwa mtazamo wao kutoka ule wa "utumwa" wa kuajiriwa na kuwa na ule wa "kifalme" wa kujiajiri na kumiliki biashara.
Walimu mbalimbali walifundisha masomo yapatayo 8 na kuwafanya wahudhuriaji kutaka DigitalBrain waandae kongomano jingine kama hilo mapema iwezekanavyo.
Wahudhuriaji wengi walitoka hapa Dar,Kibaha,Arusha,DRC-Congo na hata Ufaransa.
Habari zaidi zitafuata hapo baadaye.
No comments:
Post a Comment