Thursday, August 29, 2013

HII NDIO HISTORIA YA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA

HII NDIO HISTORIA YA MAREHEMU ASKOFU MOSES KULOLA

Marehemu Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake

MOSES KULOLA, aliyezaliwa mwaka 1928 katika familia ya watoto kumi, na kufariki mwezi Agosti 2013 katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam. Ambapo kwa sasa wamebaki ndugu zake wanne.

Moses Kulola alijiandikisha katika shule ya kwanza mnamo mwaka 1939. Shule hiyo ilikuwa inaitwa Ligsha Sukuma, ilikiwa ni shule ya Misheni. Baada ya kumaliza hapo Ligsha Sukuma Mission School, Moses Kulola akajiunga katika Idara ya  Uchoraji wa Majengo mnamo mwaka 1949. Na mwaka 1950 alibatizwa katika Kanisa la AIM Makongoro, mjini Mwanza.

 Alifanikiwa kumuoa Elizabeth na Mungu aliwajalia kupata watoto 10, ambapo kwa sasa saba (7) bado wako hai.  Alianza kazi za Umisionari mnamo mwaka 1950, ingawa alikuwa amesikia wito huo mwaka ule wa 1949!

Faustine Munishi(malebo) Moses Kulola,Emmanuel Mwasota.

 Mwaka 1959 aliajiriwa serikalini. Lakini pamoja na kuajiriwa huko Moses Kulola aliendelea na kuhubiri Injili katika Miji na Vijiji. Utumishi wake kama mwajiriwa wa Serikali ulikwisha mwaka 1962 baada ya kuwa amekabidhi nguvu, mwili na nafsi yake katika kazi ya Mungu! Ilipofika mwaka 1964 aliamua kusoma na akajiunga katika  Chuo cha Theolojia na kuhitimu katika kiwango cha Diploma mamo mwaka ule wa 1966.

Endelea kusoma historia hii kwa kubofya hapa chini 

Baada kupata Diploma hiyo hakuishia hapo bali aliendelea kusoma kwa Njia ya Posta na kupata Vyeti vingi sana kutoka Sehemu mbali mbali duniani.

Alitumikia miaka miwili kama mchungaji, 1961-1962, katika kanisa hilo la AIM na baada ya hapo akawa muumini wa Kipentekoste. Halafu akatumikia katika kanisa la TACR kuanzia 1966 hadi 1991 ambapo alijisikia kuanzisha Evangelistic Assemblie of God, maarufu kama EAGT. EAGT ni kanisa ambalo limefanikiwa kukua kwa kasi kubwa nchini hasa Tanzania, Zambia na Malawi ambapo jumla yake ni kama makanisa 4,000 yakiwa ni makanisa makubwa na madogo, na yeye Moses Kulola ndiye akiwa Askofu Mkuu na Msaidi wake akiwa Askofu Mwaisabira.

Ilikuwa sio  kazi rahisi kuendesha makanisa elfu nne (4,000) na ndiyo maana ikabidi Moses Kulola kuamua kugawanya makanisa hayo katika maeneo 34 ya kiutendaji, kukiwa na Kanda Tano ili kurahisisha kazi hiyo ya Mungu. Kila eneo na Kanda kuna mwangalizi wake.

R.I.P ASKOFU MOSES KULOLA

Source:http://pamojapure.blogspot.com/2013/08/hii-ndio-historia-ya-marehemu-askofu.html

No comments: