Tuesday, October 30, 2007

Mahakama ya kadhi Tanzania imeanza kutumika- by Mtikila


MCHUNGAJI Christopher Mtikila, amedai kuwa sheria za Mahakama ya Kadhi zimeshaanza kufanya kazi nchini kutokana na Sheikh Ponda Issa Ponda kutangaza katika Msikiti wa Mtambani kuwa yeye (Mtikila) ni kafiri na anastahili kukatwa kichwa.
Mtikila, alitoa kali hiyo jana baada ya kuelezwa na wanachama wake kuhusu suala hilo, baada ya kulisikia msikitini.
Alisema Oktoba 26 mwaka huu, wanachama wake watatu waliokuwepo katika msikiti huo ndio waliompelekea taarifa hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jana, Mchungaji Mtikila, alisema matamshi hayo ya kutaka kukatwa kichwa ni lazima ayatumie kama ushahidi katika kesi yake.
"Kama mimi nikikatwa kichwa kwa kuwa tu nimesema kuwa Mahakama ya Kadhi ni ugaidi, basi Sheikh Khalifa Khamisi, Sheikh Yahya Hussein na Sheikh Issa Ponda wao ndio watakuwa wa kwanza kukatwa vichwa vyao, kwa kuwa wao ndio wanaokula fedha za Waislamu.
"Wananchi waelewe ugaidi umeanza hata kabla ya Mahakama ya Kadhi…..je, mahakama ingekuwepo si balaa….. watu wanatumia redio kusema kichwa cha mtu kikatwe, sasa huu ni utawala gani?" alihoji Mtikila.
Kutokana na hilo, Mtikila alisema amepekea taarifa ya suala hilo Kituo Kikuu cha Polisi, lakini hakuonana na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, na kuahidi kwenda tena.
Mtikila aliwataka wananchi waungane naye na ikibidi wafanye maandamano kwa kuipinga seikali, kwa kunyamazia suala hilo ambalo ni hatari kwa taifa.

No comments: