Wednesday, January 30, 2008

Wadau wa blogu ya Sayuni.

Napenda kuwajulisha wadau ulimwenguni kote kuwa kuanzia sasa tutakuwa tunapokea picha zikiambatana na salama mbali mbali kutoka kwenu wapendwa katika Bwana.
Unachotakiwa kufanya ni kutuma picha yako yoyote unayoona inafaa kuonyeshwa hapa ikiambatana na maelezo mafupi na sisi tutairusha hapa hewani bure kabisa.
waweza kutumia email address hii hapa:
miwlc@yahoo.com

Kwa kuanzia tutaanza na picha ya mtoto Chinyemi Mbutho Chibwaye anayeishi mbezi beach jijini dar es salaam.
Yesu alisema "waacheni watoto wadogo waje kwangu msiwazuie.Maana ufalme wa mbinguni ni wao".

Mtoto Chinyemi Mbutho Chibwaye sasa amefikisha umri wa miezi 3 na week 3 na siku 3.Picha hapo juu anaonekana akiwa na miezi 3.
Anapenda kuwapa salamu wadau wote wa sayuni waliotawanyika dunia nzima.

Anapenda kuwapa mstari wa kukumbuka kutoka kitabu cha Isaya 63:7

1 comment:

Anonymous said...

HII NAYO IMETULIA!!! HONGERENI SANA