Thursday, April 30, 2009

Mbiu ya maombi

Bwana asifiwe sana,
Mlima sayuni unaomba kuwatangazia wanasayuni wote kuwa mtumishi na mtendakazi mwenzenu,mtu wa Mungu na askari hodari ndani ya jeshi la Kristo Yesu Bwana wetu mtumishi Frank Lema yu katika hali ya ugonjwa kwa muda wa wiki kadhaa.Bwana amemponya na sasa anaendelea vyema na matibabu na Mungu ameanza kumponya.Kwani alikuwa hawezi lakini sasa anaendelea vyema sana.
Mlima Sayuni bado unawaomba wanasayuni wote kumkumbuka mtenda kazi huyu asiyezimia katika maombi yenu.
Isaya 53 :1-6 I".... kwa kupigwa kwake sisi tumepona.."
Mungu awabariki sana.

Kizaa zaa Dar es salaam--Mabomu yatikisa jiji

MAMIMIA ya wananchi wamekimbia nyumba zao maeneo ya Mbagala Kuu kwa miguu hadi Tuangoma Kongowe umbali wa kilomita tatu na nusu katika Manispaa ya Temeke, kufuatia milipuko ya mabomu iliyotokea jana katika kambi ya JWTZ, iliyo Mbagala.
Akizungumza na Mwananchi, mmoja wa wananchi hao, Mohamed Said alisema hali ni mbaya watu wamefadhaika na nyumba kadhaa zimeharibiwa na wengi wao wapotezana na familia zao.
“Mimi nimepotezana na watoto wangu na baadhi ya ndugu zangu sijui waliko,” alisema.
Walipoulizwa kwamba sasa wanaelekea wapi, walisema wanakwenda kujihifadhi kwa ndugu zao wanaoishi maeneo ya Tuangoma.
Wakati huhuo, moja ya bomu lililoruka kutoka katika kambi hiyo liliangukia eneo hilo la Tuangoma na kuleta taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.
Baadhi ya watu kutoka Mbagala na maeneo mengine, walionekana wakimbilia Kitunda, Gongo la Mboto, Chanika na Mkuranga kwenda kujihifadhi wa ndugu zao na wote walikuwa wakitembea kwa miguu ili kuokoa maisha yao.
Athari za mabomu pia zililikumba eneo la Tandika Mikoroshini ambako baadhi ya vipande vya mabomu viliangukia katikati ya makazi ya watu.
Wakizungumza na Mwananchi wakazi wa maeneo hayo wanasema vipande vya bomu hilo vilidondoka eneo hilo kwa kishindo kikubwa na kufuatiwa na moto ambao hata hivyo haukuzifikia nyumba zao.
Mkazi mmoja wa Tandika, Asha Jumanne alisema kabla bomu hilo kutua mahali hapo, alilishuhudia likipita angani wakati akianika nguo za mwanae, hivyo kumfanya aache shughuli zake na kukimbia ili kuokoa maisha yake na kuwaacha watoto wake waliokuwa wamelala ndani.
Katika maeneo ya Kiwalani hali ilikuwa mbaya, baada ya mtikisiko wa bomu ulipofumua paa la kibanda ambamo vijana kadhaa walikuwa wanaangalia filamu ya kutisha ya ‘Predator’ ya Arnord Schwarzenegar.

Tuesday, April 28, 2009

Shalom

Wanasayuni.
habari za muda mrefu,imekuwa ni kipindi kirefu cha kama mwezi mzima tumekuwa hatupo hewani kwa kuwa tumekuwa katika matengenezo makubwa ya mtandao wetu wa sayuni.
Mungu ametuwezesha kusajili www.sayuni.com na muda si mrefu itakuwa hewani kwa mambo mazuri kabisa ya kupendeza.tunahitaji maombi yenu ili tuweze kufanya yote haya kwa utukufu wa Mungu.
Ndani ya sayuni.com utaweza kuchati na wapendwa sehemu mbali mbali duniani, kusikia radio za kikristo za hapa nyumbani Tanzania , mahubiri mbali mbali ya wahubiri wa hapa nyumbani na mambo mengine mengi mengi ya kujenga na kuburudisha.

Blogu yenu ya sayuni itaendelea kama kawaida kwa utukufu wa Mungu.