Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Kimara jijini Dar es Salaam Jonathani Ilunga anayekabiliwa na Kesi ya Utapeli kwenye Mahakama ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, jana aliwekwa chini ya ulinzi mkali baada ya kubaikika kuwa aliyemuwekea dhamana alikuwa ameghushi nyaraka.
Mchungaji huyo anakabiliwa na kesi ya utapeli wa mamilioni ya pesa kutoka kwa wananchi mbalimbali akiwemo Shabani Kassimu mfanyabiashara aliyedai kutapeliwa mali zenye thamani ya shilingi milioni 2.5 na mtumishi huyo wa Mungu.Baada ya kufika mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka yake, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Bi.Hellen Riwa alieleza kuwa amepokea barua kutoka kwa msajili wa kesi kwamba hati za dhamana zilizowasilishwa na mdhamini wake aitwaye Sharif Mohamed zilikuwa za kughushi, jambo lililoifanya mahakama hiyo kumfutia dhamana.Katika hali ya kushangaza Mchungaji huyo alikana mbele ya Hakimu kutokumjua Mdhamini wake Sharif ambaye inadaiwa kughushi nyaraka hizo na hivyo kuwasilisha nyaraka zake binafsi ambazo hata hivyo zilitupiliwa mbali.Baada ya dhamana yake kufutwa mchungaji huyo alitoa kioja kingine cha kugoma kutoka nje ya mahakama jambo lililowalazisha polisi kumtoa kwa nguvu na kumsweka lupango, hadi Desema 27 kesi yake itakaposikilizwa tena.
No comments:
Post a Comment