Tuesday, December 30, 2008

Mtoto umleavyo..!

Picha hapan chini ni mtoto aliyekutwa huko Coco Beach akinywa pombe huku mama yake akifurahia hali hiyo na kumuunga mkono kwa kumsifia kuwa huwa anamaliza bia chupa mbili kwa siku na wala halewi.

Wazazi tunawajibu mkubwa kwa watoto wetu hasa kuwaombea na kuwafundisha njia ipasayo katika misingi ya kibiblia.Kwa hisani ya mrokim.blogspot.com

4 comments:

Anonymous said...

Hongereni kwa kuwa na mtazamo huo.
Lakini mimi nafikiri jukumu la wazazi SI TU kuwaombea na kuwafundisha watoto njia ya malezi Kibiblia BALI PIA ni Kubadilika na kufuata hiyo misingi ya Biblia ili kuwa mifano. Mzazi mlevi hawezi fundisha mtoto mambo mema maana hayako ndani yake. Wazazi wakifuata misingi ya biblia wao wenyewe watakuwa mifano. Kumbuka MATENDO YANA SAUTI KULIKO MANENO. Wazazi wema huwa mfano wa kuigwa na watoto!
Mungu awabariki SAYUNI KWA KAZI YENU.

Anonymous said...

Ee Mungu wa mbinguni hii inaonesha ni kwa kiasi gani jinsi dunia ilivyomuacha Mungu. Mtoto huyu sio wa kulaumiwa bali ni sisi tulio wazazi na watu wazima ambao mienendo yetu kwa hakika haimpi Mungu utukufu. Tazama huyo mama unadhani anapeleka ujumbe gani hapo ????

Fikirikwanza said...

hii kazi kweli kama ndoo hivi hakuna haja ya kuwa na familia !
pombe hadi vitoto vichanga!

Anonymous said...

mtoto akiikosea jamii kiboko, mama je?, naona kama huyu mama ana kaujinga filani kanahitaji kuondolewa.