Friday, May 22, 2009

SEMINA YA UJASILIAMALI NCHINI

Ile kampuni inayokua kwa kasi kubwa hapa nchini ya DigitalBrain imeandaa semina kubwa ya wajasiliamali hapa nchini itakayofanyika hapa Dar es Salaam siku ya jumamosi ya tarehe 6/June/2009 katika ukumbi wa baraza la maaskofu Tanzania.
Semina hiyo ambayo itakuwa ni ya siku moja kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni itakuwa na lengo la kuwainua wajasiliamali wadogo na wale ambao badi hawajaanza ujasiliamali na wanataka kuingia kwenye ujasiliamali.
Kutakuwa na waalimu mbalimbali ambao ni wajasiliamali kwa vitendo.Kitu cha tofauti katika semina hiyo ni kwamba baadhi ya walimu wake ni watu wasio na elimu kubwa ya darasani lakini wanaelimu kubwa na uzoefu mkubwa wa jinsi ya kufanya ujasiliamali.Ni watu waliofanikiwa sana sana katika biashara na watashiriana na wewe utakaye hudhuria matamu na mahcungu ya ujasiliamali.
Kiingilio katika semina hiyo ni TSh. 20,000/- tu na formu za kujiunga zinapatikana katika ofisi za DigitalBrain pale Samora Avenue, Kelvin House, 2nd Floor, (jirani na ilipokuwa salamander -opposite na duka la simu la sapna).
Unaweza kusikiliza baadhi ya matangazo ya semina hiyo live kutoka WAPO Radio FM kwa kutembelea tovuti ya DigitalBrain ambayo ni www.digitalbraintz.com .
Kwa maelezo zaidi wasiliana na DigitalBrain kwa namba hii 0713-427857 au +255-713-427857 au email info@digitalbraintz.com
DigitalBrain---By the renewing of your mind...

No comments: