Monday, May 4, 2009

Tamasha la kuwachangia walemavu wa ngozi lafana Dar es Salaam


Siku ya may mosi tarehe 1/5/2009 katika ukumbi wa Diamond Jubilee hapa jijini Dar kulifanyika tamasha lililofana sana japo lilihudhuriwa na watu wachache sana.Tamasha hilo la uimbaji lililokuwa na lengo la kuunga mkono juhudi za serikali za kupinga mauaji ya ndugu zetu walemavu wa ngozi au maalibino lilipambwa na waimbaji nguli mbalimbali na vikundu vingine maarufu vya uambaji.Waimbaji kama Flora Mbasha aliyeimba kibao chake cha wanawake ni jeshi kubwa katika mahadhi ya vanga na mchiriku,Upendo Nkone aliimba Upendo wa Yesu , Christian Shushu aliiamba kibao kinachoshika chati kwa sasa cha Simama tumsifu Bwana.Boniface Mwaitege yeye alikuja na tazama matendo, Jackson Benti alimtukuza Mungu na kibaho cha Yesu mpenzi kikiwa katika mahadhi ya taarabu.Bila kumsahau Joseph Nyuki aliburudisha vilivyo na vibao vyake.
Tamasha hilo liliongozwa na mc anayechipukia kwa kasi hivi sasa na mtangazaji mwenye kipaji cha kipekee kabisa hapa Tanzania , Rita Chuwalo.Mlima Sayuni unaungana na serikali yetu katika kulaani vikali mauaji ya maalbino hapa nchini na popote pake duniani.

No comments: