Thursday, April 15, 2010

Kanisa linapojaa pomoni




Kanisa la Ufufuo na Uzima maarufu kama kanisa la kufufua misukule lililokuwa likiendeshea ibada zake katika majengo yake ya Ubungo karibu kabisa na Tanesco, limeamua kuamia katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe baada ya kuzidiwa na idadi ya watu.Kanisa hilo linaloongozwa na Mch. Gwajima...maarufu kama serious Pastor...(siriaz kwa maana ya uchapaji wa kazi) limekuwa likikua siku hata siku kwa kupokea mamia ya waumini kiasi cha kukosa mahala pa kuwaweka na hivyo kulazimika kuhamia katika viwanja vya Kawe."Kuna kipindi ilifika pale Ubungo watu walikuwa wanajaa hadi wanafika kukaa katika service road.." alisema mmoja wa watu aliye karibu na mch. Gwajima.Kanisa hilo hivi sasa linakadiriwa kuwa na waumini karibu 30,000 likidhaniwa ndio kanisa kubwa zaidi Tanzania lenye waumini wengi wanaongia ibada moja kwa wakati mmoja.Nilimuuliza mmoja wa watu walio karibu na Mch. Gwajima siri kubwa ya kujaza waumini wengi hivyo kiasi cha kujaa pomoni...akionekana mwenye kujiamini...muumini huyo alijibu kwa haraka kuwa "unajua ndugu Mtade, mchungaji ni mtu mwenye bidii sana ya kumtafuta Mungu...na pia anatumia muda mwingi sana kuwajenga kiimani washirika wake kiasi cha kuwafanya wawe na uwezo wa kujisimamia wenyewe....pia huwezi kukuta mchungaji anawatupia madongo watumishi wengine wakati wa ibada anazoendesha...yeye ni kazi tu" alisema.Mlima Sayuni unafanya jitihada kuweza kufanya mahojiano na Mch. Gwajima.

No comments: