Wednesday, April 28, 2010

Unamfahamu Nabii wa Pombe?Anaitwa nabii Tito (Nabii wa pombe- a prophet of beer) ni nabii anayehubiri watu kunywa pombe akitumia maandiko matakatifu ya Biblia na kudai kuwa Biblia inaruhusu kunywa pombe.Hufanya mahubiri yake maeneo ya posta mpya hapa jijini Dar es Salaam.
Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi tosha kwa magonjwa mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara. Dini yake aliyoianzisha inarushu watu kuoa wake wengi,kuvuta sigara na kunywa pombe.Huyu ndiye nabii Tito (a prophet of beer)
1 comment:

elinihaki said...

hizi ni nyakati za mwisho, na mafundisho mengi ya shetani yapo mitaani, watu wajiangalie sana maana maandiko matakatifu yanapindishwa sana iliwatu wakidhi tu tamaa zao. mtu kunywa pombe usingizie neno la MUNGU ni kupotoka sana na hukumu inakungoja.

mi nashauri mtu akiona hawezikuacha pombe aendelenazo akisubiri hukumu ya MUNGU, ila aspindue maandiko matakatifu.

mwisho
"msilewe kwamvinyo ambao mnaufisadi ndani yake bali mjanzwe Roho"