Monday, November 26, 2007

List of Tanzania 50 Top Church leaders

Jamani wapendwa, hivi ukitaka kujua nani wawe kwenye list ya 50 top church leaders or pastors, teachers,apostles, evangelists or prophets tutatumia kigezo gani?
1.Wingi wa watu?
2.Uwezo wa kufanya miujiza ,ishara na ajabu?
3.Uwezo wa kufundisha na kuwafanya watu wanafunzi wa Yesu?
4.Uwezo wa kifedha/ mali?
5.Muda mwingi au miaka mingi katika utumishi?
6.Maisha matakatifu yenye ushuhuda ?
7.Kujulikana sana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania?
au ni nini jamani wapendwa?

hebu tusaidieni hapa.

Baadhi ya picha za watumishi wa Mungu Tanzania.


Apostle Maboya(Ni kati ya watumishi waliokuwa wakijitambuisha kama mtume miaka ya mwanzo kabisa ya 90,kipindi hicho ukisikia mtu anajiita mtume ilikuwa si jambo la kawaida kama ilivyo siku hizi)
Pia ni mwanzilishi wa kanisa la Revival Assemblies of God Tanzania

Mama Getrude Rwakatare, Ni mmoja kati ya wachungaji wachache Tanzania wenye uwezo mkubwa kifedha, pia ni kati ya watanzania matajiri wakubwa.Anamiliki Shule za St. Marry's International.
Ni mwanzilishi wa Huduma/Kanisa la Mikocheni "B" Assemblissies of God.
Ni Mchungaji mwanamke mwenye mafanikio zaidi hapa nchini


Mwalimu Christopher Mwakasege.Ni mmoja kati ya waalimu wa injili maarufu hapa nchini ambaye huduma yake ya uwalimu inakusanya watu wengi sana katika mikutano na makongomani anayofanya sehemu mbalimbali hapa nchini.Anaongoza Huduma ya New Life Crusade/ New Life in Christ.
Mchungaji Christopher Mtikila.Ni Mchungaji wa kanisa ambalo wengi hatulijui jina lake.Ila ni mmoja kati ya wachungaji maarufu sana hapa nchini kwa miaka mingi hasa kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 90.Ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani hapa Tanzania na ni mpigania haki mashuhuri sana kwa miaka mingi.Ameshakamatwa mara nyingi sana na kushikiliwa na hata kufungwa.Amewahi pia kuishinda serikali mahakani mara kadhaa na amejizolea umaarufu sana kwa uwezo wake wa kuongea bila uwoga.Pia ni muhubiri na mwalimu wa miaka mingi wa Injili.


Askofu Zakaria Kakobe wa Full Gospel Bible Fellowship.Ni mmoja kati ya wachungaji maarufu sana hapa nchini.Anafahamika kwa kuwa na pengine kanisa la kiroho la mahali pamoja kubwa zaidi kwa idadi ya watu pengine kuliko mtumishi mwingine hapa nchini.


Ibada zake za kwenye TV za miujiza kwa miaka mingi zinawavutia wengi.


Mtume Veron Fernandez wa Agape Ministry.Ni mmoja kati ya watumishi wa kwanza kabisa kuhubiri katika Television na kumiliki kituo cha television hapa Tanzania.Anamiliki kituo cha ATN kituo cha kwanza cha kikristo hapa Tanzania.
amejipatia umaarufu mkubwa sana kwa mahubiri yake ndani na nje ya nchi.
Askofu Moses Kulola wa Evangelist Assemblies of God Tanzania.Ni mmoja kati ya watumishi waliotumika muda mrefu zaidi pengine kuliko wengi tunaowaona siku za leo.Ametumika kwa karibu miaka 60 akihubiri injili kutoka vijijini hadi mijini hapa nchini na nje ya nchi.Aina ya injili yake na style ya mahubiri yenye kupenya ndani ya nafsi imekuwa ikiwagusa sana watu wengi.Ni muhubiri pengine mwenye watoto wengi wengi wa kiroho kuliko yeyote aliyewahi kutokea tanzania.Kanisa lake limesambaa karibu kila kona ya Tanzania

Nabii GeorDavie wa GeorDavie Ministry iliyoko Arusha ni mmoja ya watumishi wanaokuja kwa kasi sana hapa nchini hususani mjini Arusha.

Huduma yake ya uponyaji na miujiza imekuwa ikipata umaarufu mkubwa sana hapa nchini.


Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Mission na Huduma ya Hakuna lisilowezekana.
Ni Mtumishi wa kwanza kumiliki kituo cha Radio cha kiroho hapa tanzania (WAPO Radio FM) na gazeti la kwanza la kipentekoste (Msemakweli).
Amejizolea umaarufu mkubwa kwa ibada zake za maombezi anazoziendesha na huduma ya hakuna lisolozekana.Pia ni mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste Tanzania (PCT).
Amejizolea umaarufu serikalini hadi kuteuliwa kwenye tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi.
Naomba ieleweka kwamba hawa waliotajwa hapa kwa picha haina maana ndio top Gospel Preachers/ Watumishi wakubwa kabisa hapa Tanzania bali ni mfano tu wakiwakirisha wengine waliopo hapa nchini.

12 comments:

Anonymous said...

KAKA MTADE, HAKUNA MTU ANAWEZA KUWA RANK WATUMISHI WA MUNGU KWA KIGEZO CHOCHOTE MAANA ALIYEWAPA HUDUMA NDIYE MWENYE UWEZO WA KUTOA RANK KAMA APENDEVYO MWENYEWE.

Anonymous said...

List iwe hivi

1. YESU KRISTO WA NAZARETH
2. YESU KRISTO WA NAZARETH
3. YESU KRISTO WA NAZARETH
4. .....

.
..
..

50. YESU KRISTO WA NAZARETH

Anonymous said...

hiyo list unayotaka kutengeneza ni kama hii hapa

http://www.thechurchreport.com/mag_article.php?mid=875&mname=January kwa america

na hii hapa kwa nigeria

http://www.onlinenigeria.com/links/adv.asp?blurb=110


wala hakuna kitu kisicho cha kiroho

Anonymous said...

Hivi Mzee Wetu Moses Kulola bado anaendelea kuhubiri kama kipindi kile miaka ya 80 na 90?
Aisee nakumbuka huyu mzee anapiga gospel si mchezo.Nasikia kuna kioindi aliwahi kuja huku Marekani.
Nadhani Katika hiyo list Mzee kululo lazima awe # 1.
Wengine siwafahamu vizuri sana.

Chris, TX

Anonymous said...

Kuweka orodha ya watumishi siyo vibaya, lakini kutumia maneno kama "amejizolea umaarufu" si vema katika kazi ya Mungu. Ni vema watumishi wa Mungu waonekane vivyo kama watumishi, ukianza kuweka vyeo basi wanakuwa watawala. Pia kipimo cha ubora kinawekwa na Mungu aliye bosi wao. asante

Anonymous said...

Mh kwakweli katika mambo ambayo siwezi kuyaongelea sana ni maswala ya hao watumishi hapo juu, ila naamini kwamba nabii wa kweli na mtumishi wa mungu wa kweli ambaye sina mashaka nae wala bifu lolote nae naninamkubali kutoka rohoni na miujiza yake naikubali pamoja na mafundisho yake ambaye nikiwa popote lazima nimwambie pia hana tabia ya kujisifia halafu anajulikana dunia nzima hata kuzimu wanamtambua aisee kwangu nabii ni YESU KRISTO peke yake wengine sina lolote la kusema maana sijawahi kuona miujiza yoyote kwao zaidi ya kusifiwa na watu wenye matatizo na shida mbalimbali especialy wenye sicological problem.

Anonymous said...

NAWASAKIMU WOTE KATIKA JINA LA
YESU KRISTO MWOKOZI WA ULIMWENGU
KATIKA WACHANGIAJI WENGI WANAWAFAHAMU KWA KARIBU BAADHI YA WATUMISHI NI VEMA KATIKA MCHANGO MTU ASIWEKE USHABIKI BALI ASEME KWELI ILI HATA KAMA KUNA MADHAIFU AU MAPUNGUFU KATIKA MTUMISHI ALIYEONGELEWA AWEZE KUSAIDIKA KWANI MUHUSIKA ATAKAPOKUWA ANASIKIA UPANDE MMOJA WA HABARI ZAKE KUNA HATARI YA KUJIINUA NA KIBURI CHA UZIMA NI VEMA KUELEZA HATA MAENEO AMBAYO NI NJIA YA KUMSAIDIA MTU HUYO NA KUFANYA HIVYO HAKUNA LAANA KWAMBA UMEMNYOOSHEA KIDOLE KUHANI WA MUNGU ASANTE KWA LEO MIMI
THOBIASI NICHOLAUSI MOSHA
MCHUNGAJI MTENDA KAZI
MPONDA TAG CHURCH
SIMU +255 776 341971
Email thobiasi@yahoo.com

Anonymous said...

SALAMU WATUMISHI WA MUNGU POPOTE
DUNIANI JINA LANGU NAITWA
THOBIASI NICHOLAUSI MOSHA NI MTUMISHI MTENDA KAZI KATIKA KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD MPONDA TEMEKE DAR ES SALAAM
NAOMBA MUNIKUMMBUKE KATIKA MAOMBI KWANI NIMEANDAA TIMU YA VIJANA KWA AJILI YA KUSHUHUDIA NYUMBA KWA NYUMBA NA MTU KWA MTU KWA SIKU TATU NI MATUMAINI YANGU KUWA MUNGU AHUSIKE NA WATU WA KIJIJI CHA MPONDA -
-ROHO YA TOBA IWE NDANI YAO
-HOFU YA MUNGU ITAWALW WAKATI WA HUDUMA
-NGUVU ZA MUNGU ZITEMBEE NA WATENDAKAZI WAKATI WOTE
-KAZI ZA SHETANI ZIHARIBIWE
-KRISTO AJIPATIE MATEKA
MUNGU AWABARIKI KWA MAOMBI YENU
MIMI
THOBIASI
SIMU 0776 341971

lusingu said...

Bwana YESU asiwe. mimi ninaamini kabisa vipo vigezo vinavyoweza kutambilisha mtumishi wa mungu, lakini vigezo hivi visimamie utakatitifu, kumpa Mungu utukufu peke yake, kuihubiri injli ya yesu kristo kama inavyo sema bilila kuonyesha kwamba mtumishi anasehemu katika utukufu wanguvu za Mungu alie hai.

Anonymous said...

bwa na Yesu apewe sifa. mimi ninaamini kabisa kwamba

lusingu said...

Bwana yesu asifiwe sana. mi ninaitwa Lusingu charles. kwaupande wangu kigezo au vigezo vyakumtambua mtumishiwa MUNGU ni maisha ya utakatifu tena yenye ushuhuda pamoja nakulihubiri neno katika uhalisia wake ili kuwaleta wengi kwa YESU. namtumishi huyu amrudishie MUNGU utukufu kila MUNGU anapojidhihirisha kwenye huduma.

Kajema said...

Kila mtumishi wa Mungu ana alichotumwa kifanyika katika kanisa ni vigumi sana kupanga list kama unavyotaka. Kila mmoja yupo kwa ajili ya kuwakamirisha watakatifu hata mwali wa Kristo ujengwe.