Wednesday, September 15, 2010

Wasiwasi wa ugaidi Kampala


Tangu kutokea kwa milipuko ya mabomu huko kampala miezi miwili iliyopita na kuuwa watu karibu 76, mji wa Kampala kwa sasa umekuwa na ulinzi wa hali ya juu.
Tulikutana na hali hiyo tulipoenda "mlimani city" ya Kampala na tulilazimika kusimama kwa dakika kadhaa ili kukaguliwa kwa umakini wa hali ya juu hata pale tulipojitambulisha kuwa sisi ni watumishi wa Mungu kutoka Tanzania.

Watu wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi mkubwa sana.
Sayuni tunasema BWANA asipoulinda mji waulindao wafanya kazi ya bure...

No comments: