Kwako mwanangu .....................
Yawezekana ya kuwa hunijui lakini najua kila kitu juu yako. Zaburi 139:1
Najua kukaa kwako na kuondoka kwako. Zaburi 139:1
Nazifahamu njia zako zote. Zaburi 139:3
Hata nywele za kichwa chako najua hesabu yake. Mathayo 10:29-31
Kwa sababu uliumbwa kwa mfano wangu. Mwanzo 1:27
Ndani yangu unaishi na kutembea. Matendo 17:28
Kwa sababu wewe ni uzao wangu. Matendo 17:28-1
Nalikujua kabla sijakuumba. Yeremia 1:4-5
Nalikuchagua wewe nilipopanga kuumba ulimwengu. Waefeso 1:10-12
Hakuna makosa kwa sababu hata siku zako zimeandikwa katika kitabu changu. Zaburi 139:15-16
juu ya kuzaliwa kwako na mahali utakapokaa. Matendo 17:26
Wewe uliumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Zaburi 139:14
Nalikuunga pamoja katika tumbo la mamako. Zaburi 139:13
Nikakutoa tumboni mwa mama siku uliyozaliwa. Zaburi 71:6
Nimekosa kujulikana na kuwakilishwa nao wasionijua. Yohana 8:41-44 Sijakasirika lakini upendo wangu umekamilika. 1 Yohana 4:16
Na ni mapenzi yangu kukuonyesha upendo wangu kwako. 1 Yohana 3:1
Hii ni kwa sababu wewe ni mwanangu na mimi ni babako. 1 Yohana 3:1 Nimekupa mambo ambayo babako wa duniani hawezi kukupatia. Mathayo 7:11 Kwa sababu mimi ni baba mkamilifu. Mathayo 5:48
Kila kipawa kizuri hutoka mikononi mwangu. Yakobo 1:17
sababu mimi nakupa mahitaji yako yote. Mathayo 6:31-33
Mipango yangu kwa ajili yako ni kwa sababu nakupenda kwa upendo wa milele. Yeremia 31:3
Mawazo yangu kwako hayawezi kuhesabika ni kama mchanga wa baharini. Zaburi 139:17-18
Najifurahisha na vipaji vyako. Sefania 3:17
Sitaacha kukutendea mema. Yeremia 32:40
Kwa sababu wewe ni mali yangu ya thamani. Kutoka 19:5
Napenda kukupanda katika nchi kwa moyo wangu na nia yangu. Yeremia 32:41 Napenda kukuonyesha mambo makuu usiyoyajua. Yeremia 33:3
Ukinitafuta kwa moyo wako wote utanipata. Kumbukumbu 4:29
Nitegemee mimi nami nitakupa haja za moyo wako. Zaburi 37:4
Kwa sababu ni mimi ambaye huwapa watu haja za moyo wao. Zaburi 37:4 Maana ni mimi ninayekupa hayo mahitaji yako. Zaburi 2:13
Ninao uwezo wa kufanya makuu kuliko uyawazayo. Waefeso 3:20
Kwa sababu mimi ndiye niwezaye kukuimarisha. 2 Wathesalonike 2:16-17
Tena mimi ndiye ninayewapa wanaohitaji mahitaji yao. Zaburi 2:13
Ninao uwezo wa kukutendea makuu kuliko unayofikiria. Waefeso 3:20
Kwa sababu mimi ndiye ninayekupa nguvu. 2 Wathesalonike 2:16-17
Tena mimi ni baba anayekufariji wakati wa shida yako. 2 Wakorintho 1:3-4 Wakati moyo wako umevunjika niko karibu kukufariji. Zaburi 34:18
Kama mchungaji anavyomchukua mwanakondoo nimekuchukua ndani ya moyo wangu. Isaya 40:11
Nitayafuta machozi katika macho yako. Ufunuo 21:3-4
Na maumivu yako uliyoyapata hapa duniani nitayaondoa. Ufunuo 21:3-4
Mimi ni babako na ninakupenda kama nimpendavyo mwanangu Yesu Kristo. Yohana 17:23
Kwa sababu ndani ya Yesu upendo wangu huonekana. Yohana 17:26
Yeye huniwakilisha kuweko kwangu. Waebrania 1:3
Alikuja kuonyesha kuwa mimi niko upande wako si kinyume chako. Warumi 8:31
Na kukuambia ya kuwa sitakuhesabia makosa yako. 2 Wakorintho 5:18-19
Yesu alikufa ili mimi na wewe tuunganishwe pamoja. 2 Wakorintho 5:18-19 Kifo chake kilionyesha upendo wangu kwako. Yohana 4:10
Nilitoa yote ninayopenda ili nipate wewe na upendo wako. Warumi 8:32 Ukipokea zawadi ya mwana wangu ndipo unanipokea mimi.1 Yohana 2:23
Hakuna chochote kitakachoweza kukutenganisha na upendo wangu. Warumi 8:38-39
Karibu nyumbani na nitaandaa karamu ambayo haijaonekana huku mbinguni. Luka 15:7
Nimekuwa baba yako na nitaendelea kuwa baba yako milele. Waefeso 3:14-15 Swali langu kwako, je, utakubali kuwa mwanangu? Yohana 1:12-13
Nakungojea wewe. Luka 15:11-32
NAKUPENDA HUYU NI BABAKO WA MILELE-ISAYA 9:6
Muhuri(Roho mtakatifu)NDIMI NIKO AMBAYE NIKO Kutoka 3:14
Imeletwa na Yesu-(neno la Mungu-Yohana 1:1)
Kalenge