Friday, February 29, 2008

Eeee Mungu epusha uovu huu Tanzania

Dunia imekwisha na inakoelekea ni kubaya kuliko ilipotoka. Sielewi nini maana yake haya tuyaonayo humu duniani ila sauti moja yaniambia, tuyaonapo hayo ujue kwamba ule mwisho umekaribia. Wapendwa kila aaminiye kwamba Yesu ni mwana wa Mungu basi na amshike sana huyo Yesu asimwachilie.
Uko uovu unaofanyika hapa Norway sehemu iitwayo STORĂ…S pembeni mwa mji mkuu Oslo, ambao kwa kweli Sodoma na Gomora ni afadhali. Huko huwa wana summer parties ambazo watu hutembea uchi kama walivyozaliwa na kusherekea hali hiyo pasipo haya. Kwa hali kama hii, kwa nini hasira ya Mungu isiwake juu ya uso wa dunia? Eee Mungu iepushe Tanzania na uovu huu!

Angalia picha hizo na kisha shuhudia hii video clip hapa chini. (Ipo kwa kinorway lakini - mtangazaji anamuhoji huyo jamaa anajisikiaje kuwa hivyo na wanafanya nini hapo? Jibu la jamaa ni kwamba wako wana-enjoy na kufurahia hali hiyo na karibu kila mwaka yupo hapo kwake hii ni mara ya tatu. Hapo ilikua ni saa tano asubuhi)

1 comment:

Mtade said...

Aisee Chalukulu hii youtube imenichekesha sana japo inasikitisha kwa kweli.
aisee inamaana kuna watu wanaishi kama wanyama huko duniani..du..!