Monday, February 11, 2008

Mchungaji Getrude Rwakatare akabidhi kanisa TAG?

Habari zilizotufikia zinasema kuwa mch. Getrude Rwakatare amemwandikia barua askofu mkuu wa TAG , Mwenisongole kumjulisha nia yake ya kulikabidhi kanisa hilo kwa TAG kwa kipindi chote ambacho yeye atakuwa mbunge ila kwa sharti kwamba atampendekeza yeye mchungaji atakaye simamia kanisa kwa kipindi hicho chote.
Katiba ya TAG hairuhusu mchungaji yeyote kuwa mwanasiasa hali inayoonekana kuwa ngumu kwa Mch. Rwakatare.

Hata hivyo Jumapili iliyopita Mch. Rwakatare amekaririwa akikanusha vikali habari hizi kuwa amelikabidhi kanisa kwa TAG wakati akihubiri katika ibada ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa mbunge iliyofanyika kanisani hapo mikocheni "B" Assemblies of God.

Baadhi wa washirika wa kanisa hilo wamesema kuwa kuna mgawanyiko umeanza kujitokeza miongoni mwa washirika na baraza la wazee hasa kwa wale wanaounga mkono uamuzi wake wa kujiingiza katika siasa na wale wanaompinga.

Sayuni blog itawaletea habari zaidi kadri tutakavyopata habari kutoka katika vyanzo vyetu.

No comments: