Friday, February 8, 2008

Umuhimu wa Mch. Rwakatare waanza kuonekana bungeni

Ile dhana kuwa siasa na dini haviwezi kuchangamana imeanza kuonekana kukosa msingi baada ya suala la richmond na kutuhumiwa kwa waziri mkuu E. Lowasa,waziri wa nishati na madini N. Karamagi na waziri wa east africa I. Msabaha kuingiza hisia za watu kumcha Mungu kwa kiwango kikubwa.Nadhani jana tarehe 7/2/2008 ni siku pekee ambayo Mungu na watu kumwofu Mungu kumetajwa sana bungeni kuliko siku yeyote.
Watu wengi wameanza kuona umuhimu wa mch. Rwakatare bungeni.

Shime watu wa Mungu tunahitaji wacha Mungu wengi sana waingie bungeni ili kuondoa kila aina ya ufisadi katika nchi yetu.

2 comments:

Anonymous said...

Watu wa Mungu ni muhimu sana kuwa bungeni -tena wanahitajika hasa kuwa wale walio waombaji na wanojilisha neno la Mungu kwa bidii.Hutuwezi kukimbia siasa watu wa Mungu kwa sababau sera zinapotungwa pia zinawaathiri watu wa Mungu positively ama negatively watu wa Mungu wanatakiwa kuthibiti maswala kama hayo. Cha msingi ni kwamba kuwepo uongozi wa Mungu kuingia kwenye siasa. Mtu asikurupuke tu na kujiingiza kwa sababu ya Tamaa. Kuingia kwenye siasa napo ni wito -Usiingie kwenye siasa kama hujaitwa la sivyo utashindwa na kukosa ulinzi wa Mungu. Kama Mungu akisema nenda kapande mbegu ya Kristo. Siasa sio laini kuna mapambano mengi na vita vya kila aina pengine hata kuzidi kazi ya uchungaji -Mungu lazima awe ame-approve. Mama Rwakatare ni mtu anayependa kazi ya Mungu pia anapenda maendeleo ya watu-yamkini Mungu anataka aingie bungeni awqakilishe kanisa na kwa muda maalumu naamini itawezekana na inafaaa baadae kazi aliyotumwa ikiisha arudi kazi ya uchungaji full time -ushauri wangu ni kwamba asingeacha kanisa kabisa anaweza kuwa part time sio kuacha kabisa -hakuna kosa lolote kuwa mchngaji na mbunge sana sana tofauti ni uzito tu wa kazi. Kanisa linatakiwa kuwa na hekima sana jinsi ya kumshauri mchungaji na wasiwe na lawama wala kuleta mgawanyiko
Mungu awabariki
Mimi ni edith Hillary Mwita -Boston USA.Nimeokoka !

Anonymous said...

Ulichosema dada Edith ni cha kweli kabisa,nadhani tatizo hapa ni kuwa watu bado hawajafahamu kuwa siasa na dini huwezi kuvitenganisha.
Mfalme Daudi alikuwa mwanasiasa na kiongozi wa kiroho.Agano la kale lote tunaonana uhusiano wa siasa na dini kwa ukaribu zaidi.
mimi nadhani tunahitaji kujipanga na kudefine kanisa liingiaje ndani ya siasa na sio kukataa kuwa viwili hivi haviwezi kuchangamana.

Mwakisole,Kigoma,
Tanzania