Monday, February 11, 2008

Mizengo Pinda : Waziri mkuu mpya wa Tanzania

Rais Jakaya Kikwete amemtea na kumwapisha mh. Mizengo Pinda kuwa waziri mkuu jumamosi hii kuchukua nafasi ya Edward Lowasa aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond maarufu kwa jina la "richmoduli".

Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Waziri mkuu mpya wa Tanzania mh. Mizengo Pinda aliyeshikilia Biblia Takatifu akila kiapo.
Leo hii rais Kikwete anatarajiwa kutangaza baraza jipya la mawaziri baada ya kulivunja baraza lote lilikuwa chini ya waziri mkuu wa zamani Lowasa.


Waziri mkuu mh. Mizengo Pinda akikumbatiana na Waziri mkuu aliyejiuzulu mh. Edward Lowasa

No comments: