Wednesday, January 7, 2009

DigitalBrain waanza kusikika live kwenye Internet

Ile kampuni inayokuja juu na kwa kasi katika maswala ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya DigitalBrain imeanza kurusha vipindi vyake vya radio kupitia kwenye mtandao live.
Akizungumza na Sayuni , mkurugenzi wa ufundi wa kampuni hiyo Bw. Marco Salimu amesema kuwa wameamua kurusha vipindi hivyo vya radio kwenye mtadao ambavyo hurushwa na radio Wapo FM ya jijini Dar es Salaam ili kuwapa fursa wasikilizaji walioko maeneo kusikofikika na mawimbi ya radio hiyo kuweza kupata elimu hiyo inayotolewa na wataalamu wa kampuni hiyo.
DigitalBrain ni kampuni ya wazawa inayojihusisha na maswala ya ICT iliyojizolewa umaarufu mkubwa miongoni mwa jamii kwa hivi sasa kutokana na kipindi hicho.Kipindi hicho hurushwa na radio hiyo kila siku ya jumatatu saa mbili kamili usiku hadi saa tatu kamili.
Waweza kusikiliza matangazo hayo hapa kwenye link hii www.digitalbraintz.com

Mungu awabariki DigitalBrain kwa kazi njema.

2 comments:

Anonymous said...

Tumewasikia watumishi ndani ya WAPO RADIO kupitia website yenu. Vipi je mtatuwekea na vitu vingine vya WAPO au ndo promotion za kampuni yenu tu?

pius said...

Haya ni mambo mazuri, Mungu awawezeshe zaidi.Hongera Mbutho na wadau wote wa digitalbrain.