Tuesday, January 20, 2009

DigitalBrain yajitolea kuidhamini mlima sayuni

Ile kampuni kubwa ya kizalendo ya DigitalBrain sasa imejitolea kuudhamini mlima sayuni kwa kuutengenezea website yake itakayogharimu zaidi ya dola 5000.Website hiyo itakayokuwa ni web portal ya aina yake kuwahi kutokea hapa Tanzania itakuwa na kila kitu kinachopaswa kuwapo katika website za kisasa.Kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja na nusu mlima sayuni umekuwa ukipatikana kwenye blog na kwa kuwa kwenye blogu lakini sasa DigitalBrain wameamua kugharamikia shughuli zote za kuitengeneza website hii kubwa na ya kipekee kabisa barani Afrika.
Katika website hiyo itakayokuwa tayari kabla ya mwisho wa mwezi huu,kutakuwa na mahubiri LIVE mbali mbali,muziki wa injili na pia utawaona LIVE wahubiri mbalimbali na wachungaji mbalimbali wanaotumiwa na Bwana hapa nchini.
Pia utaweza kusikiliza radio mbalimbali za kikristo kama Radio WAPO FM, Praise Power FM na Upendo FM zote za jijini Dar.
Kwa wale walio ughaibuni kaeni mkao wa kupokea baraka hizi ambazo wengi mmekuwa mkizisubiria kwa muda mrefu.
Pia utaweza kushiriki mijadala mbalimbali ya wapendwa na mambo ya kisiasa na kijamii.Kuchat na wapendwa mbalimbali,kununua na kuuza bidhaa mbalimbali, kupata taarifa za nyumba za kupangisha na kununua, na mambo mengine mengi mengi mengi ya kujenga.
Kwa hivi sasa DigitalBrain wanarusha vipindi vyao kupitia radio WAPO FM na unaweza kuwasikiliza LIVE kupitia mtandao wao wa http://www.digitalbraintz.com/ . Waweza kusikiliza kipindi chao kilichorushwa jumatau ya jana na jumatatu zingine zilizopota.
Akiongea na Mlima sayuni mkurugenzi wa Ufundi wa DigitalBrain Mr. Marco Salimu amesema kuwa wameamua kufanya kitu kizuri kwa ajili ya mwili wa Kristo na wamejitolea kiasi hicho cha fedha kwa kuwa wanaamini katika kutoa na kubarikiwa katika kipimo cha kujaa,kushindiliwa,kusukwasukwa kumwagika jinsi Bwana YESU atakavyowabariki.
...DigitalBrain..By the renewing of your mind..

No comments: