Tuesday, January 6, 2009

MWIMBAJI WA INJILI FANUEL SEDEKIA KATUTOKA. HABARI ZA KUSIKITISHA ZIMEINGIA SASA HIVI KWAMBA MWIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI, FANUEL SEDEKIA, AMEFARIKI DUNIA JANA KATIKA HOSPITALI YA PORIYA TIBERIA, HUKO ISRAEL.
HABARI ZINASEMA MAREHEMU ALIKUWA AMELAZWA KWA WIKI TATU HOSPITALI HAPO AKISUMBULIWA NA KISUKARI PAMOJA NA NIMONIA. ALIKUWA HUKO KATIKA MSAFARA WA MAHUBIRI NA MCHUNGAJI MWAKASEGE.

MIPANGO YA KUULETA MWILI WAKE NYUMBANI KWA MAZISHI UNAFANYWA NA TUTAENDELEA KUWAFAHAMISHA HABARI ZINAPOTUJIA. KWA SASA KINACHOFAHAMIKA NI KWAMBA MSIBA UTAKUWA NYUMBANI KWAKE ARUSHA NA ATAKAPOZIKIWA BADO HAIJAJULIKANA KWANI YEYE KWAO NI KIGOMA.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA...JINA LA BWANA LIBARIKIWE..
source: swahilitime.blogspot.com

1 comment:

Anonymous said...

Hongera kwa kufanya kazi ya Mung kwa kipind chako kifupi dniani.

I love you brother,RIP