Saturday, January 10, 2009

KWA HERI SEDEKIA

Hakika mtumishi wa Mungu alale kwa amani!

Kama kuna watu walibariki moyo wangu ni Fanuel Sedekia na naomba niamini vivyo hivyo kwa mioyo ya watu wengi kama jinsi ambavyo umati wa watu ulivyojihudhurisha pale kwenye viwanja vya Sheikh Amri abeid Karume, Arusha mjini. Mtu huyu alipendwa na wengi na huo ni udhihirisho tosha namna ambavyo mwili wake uliheshimiwa kwenye kuagwa na hata mazishi yake.

Yatosha kwa siku maovu yake na Bwana ampe faraja haswa mjane na watoto wake pasipo kusahau wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja ama nyingine!!

Hebu basi tujikumbushe walao kwa nyimbo hizi wakati tukiendelea na maombelezo.

No comments: