Tuesday, July 21, 2009

Kadhi ni nani?

Ndg mpendwa.

Wakristo tunayo HAKI ya kushiriki kyk kutazama mahakama ya kadhi kabla ya kuiruhusu/kukubali itumike ktk kutoa hukumu hapa nchini Tanzania.
Hii ni kwa sababu itakapoanza kutoa hukumu hapa nchini haitakuwa juu ya waislamu tu bali hata kwa wengine kwa sababu za kizazi.Hii ni kwa maana wapo wapo wakristo waliooa na kuzaa na waislamu pia wapo waislamu waliooa na kuzaa na wakristo hivyo hukumu kupitia vitabu vya dini ya kiislamu haigusi waislamu tu bali hat jamii ya wakristo.
Ni vema tuanze kwa kumtazama huyu mtu aitwae KADHI je ni nani na anabeba sifa zipi ili tuwe huru kumpa madaraka ya kuhukumu.
BIBLIA;LUKA 18;2-6
(Akasema palikuwa na KADHI katika mji fulani hamchi Mungu wala hajali watu.Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane aliyekuwa akimwendea endea akisema.Nipatie HAKI na adui wangu Nae kwa muda alikataahalafu akasema japokuwa simchi Mungu wala sijali watu lakini kwa kuwa mjane huyu ananiudhi nitampatia haki yake asije akanichosha kwa kunijiadaima.Bwana akasema sikilizeni anayosema yule KADHI dhalimu).
Katika neno hilo tunazipata sifa kuu nne za KADHI nazo ni


1HAMCHI MUNGU.
2.HAJALI WATU.
3HUTOA HAKI PALE ANAPOSUMBULIWA.
4.NI DHALIMU.

Ikiwa kama ameshindwa kumpa HAKI yake mjane ambaye ana HAKI YA KUSAIDIWA, Je ataweza kutoa HAKI ya HUKUMU ya KWELI hapa TANZANIA?

HAPANA KWA SABABU HANA SIFA ZINAZOSTAHILI.

swala jingine la kujifunza ni kuwa waislamu wanalalamika kuwa serikali imewanyima HAKI YA KUABUDU(majira 7/7/2009. je ni haki gani hiyo ya kuabudu wakati kila siku tunasikia AZANA misikitini nao huenda huko kuabudu?
Moja ya mikakati ya serikali yetu hapa tanzania katika kulinda amani na utulivu imetoa UHURU WA KUABUDU KWA WATU WOTE kama ilivyo kwa watu wote je ni uhuru gani wa kuabudu waislamu wamenyimwa?

Ikiwa kama kweli wamenyimwa basi wasiende misikitini lakini ikiwa hawajanyimwa basi watubu kwa watanzania kwa kusema uongo.ikifuatiwa na BAKWATA kutengua kauli hiyo katika gazeti la majira 7/7/2009.Vilevile waislamu huko UK nao wanalalamika kwa kunyimwa haki(Daily News july 15,2009 pg 25.je unajifunza nini katika hili???


Yafaa kutambua kuwa tuko kwenye nyakati za KUNG'ANG'ANIA ULICHO NACHO KWA KUKISHIKIRIA SANA ILI ASIJE MWOVU ..........................
Mkristo yafaa kutembea huku TAA ikiwaka ili kutazama hatua tunazopita kama tunakanyaga mahali sahihi au la.
Hivyo kwawakristo wote wanaoiamini BIBLIA hapa duniani yafaa kufahamu kuwa KRISTO NI MWISHO WA SHERIA.
RUMI 10;1-4
(Ndugu zangu nitakayo sana moyoni mwangu na dua yangu nimuombayo Mungu ni kwa ajili yao ili waokolewe.Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudikwa ajili ya Mungu lakini si katika MAARIFA.Kwa maana wakiwa hawaijui haki ya Mungu na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe hawakujitia chini ya haki ya Mungu.Kwa maana KRISTO NI MWWA SHERIA ili kila aaminie ahesabiwe HAKI.

NA BARAKA ZA MUNGU MWENYEZI,ZA BABA,ZA MWANA NA ZA ROHO MTAKATIFU ZAWASHUKIE NA KUKAA NANYI DAIMA.
AMEN.


Charles Kabaka

7 comments:

Anonymous said...

hello... hapi blogging... have a nice day! just visiting here....

Anonymous said...

Ukitaka kujua maana au tafsiri ya kitu jaribu kutafuta kimapana,uliza na pekua kwenye vitabu vingi. Hiyo tafsiri uliyoitoa hapo haikidhi maana halisiya kadhi. Naomba uwatafute wajuzi ili usipotoshe watu

Anonymous said...

kitu ambacho mimi nilikuwa kutafuta maana, shukrani

Anonymous said...

I just added your website on my blogroll. I may come back later on to check out updates. Excellent information!

Anonymous said...

I just added your website on my blogroll. Really enjoyed reading through. Excellent information!

Anonymous said...

Really great article with very interesting information. You might want to follow up to this topic!?! 2011

Anonymous said...

KADHI NI HAKIMU KWA NJIA ZA HAKI,ANAESHURUTISHWA NA SHERIA ILIYOMO KWENYE KITABU CHA MWENYEZI MUNGU.sisi kama waislamu tunaamini vitabu vinne vilivyopewa mitume rehema na amani ziwashukie.1)DAUDI{DAVID.A.S.}ZABURI:MAWAIDHA,2)MUSA{MOSES.A.S}TAURAT:SHARIA,3)ISSA BIN MARYAM{JESUS A.S} INJIL:HABARI NJEMA ,4] MOHAMMED{S.A.W]>QUR'AN:SHARIA,NA NIKITABU KILICHOKUSANYA YOTE YALIKUWA KABLA YAKE{MOHAMMED.S.A.W.}KATIKA VITABU WALIVYOPEWA MITUME.K.V.KATIKA QUR'AN,KUNA HABARI ZA MUSA .A.S NA FIRAUN,ISSA/YESU .A.S.,SULEIMAN/SOLOM .A.S. NA DAUDI .A.S,IBRAHIMU .A.S.,NUHU.A.S.,YUSUFU .A.S,YUNUS.A.S.,NA WENGINE WENGI..YOTE HAYA MWENYEZI MUNGU ANAMSIMULIA MTUME S.A.W{MOHAMMED} ILIPATE KUZINGATIA YALIOWAFIKA MITUME WENZAKE NA PIA SISI KAMA UMMA WAKISLAMU, TUZINGATIE NA KUFWATA AMRI ZAKE.
...narudia tena"kadhi ni kiƶngozi anaeshurutishwa na sharia,zile ambazo anapo hukumia mtu afwate kama ilivyo kutoka kitabuni{QUR'AN:IMEKUSANYA YALIYOMO Katika vitabu vilvyotangulia,na pia imekusanya kila yanayofungamana na maisha yetu}.
Lakini kama mtu anahukumu kinyume kama ilivyo kwa mataifa mengi,atakuwa ana dhulumu raiya,ndiyo maana sisi kama waislamu kusema kila mara twadhulumiwa,kwani hizi sharia za inchi zimetumgwa na watu kutoka kwa vichwa vyao pasina kufwata kitabu cha mwenyezi...'KWA HIVYO NDUGU! Soma vizuri uelewe mambo yalivyo.asanteni.