Monday, August 16, 2010

Mchungaji atuhumiwa kwa ubakaji

Hii ni aibu nzito kwa Mchungaji Michael Ngilangwa (35) ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Pomerin, Wilayani Kilolo, Mkoani Iringa kupandishwa kizimbani mwishoni mwa wiki iliyopita akituhumiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa denti wa kidato cha kwanza ili amsaidie kujua somo la Kiingereza.

Mchungaji huyo wa roho za watu alijikuta akikwea kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Iringa na kusimamishwa mbele ya Hakimu Martha Ngaze ambapo mwendesha mashitaka wa Takukuru mkoani hapa, Imani Nitume alisema Ngilangwa ni mwajiriwa wa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa.

Alidaiwa kuwa, pamoja na kuomba rushwa ya ngono Ngilangwa anatuhumiwa kutaka kumbaka denti huyo (Jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili), mwenye umri wa miaka 14, hivyo kosa hilo kuwa la pili.

Mwendesha mashitaka Nitume aliongeza kusema kuwa, Mchungaji Ngilangwa anashitakiwa kwa kuvunja kifungu cha 25 cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa katika tukio hilo lililotokea Agosti 11, mwaka huu katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Mianzini mjini Iringa.


Alidai kuwa, Mchungaji Ngilangwa akiwa na mwanafunzi huyo ndani ya nyumba hiyo ya wageni, aliomba rushwa ya ngono kutoka kwa denti huyo kwa ahadi atamsaidia somo la Kiingereza na Biblia pamoja na kumpatia mahitaji yake mengine madogo madogo awapo shuleni hapo.

Wakiongea na gazeti hili mara baada ya mtumishi huyo wa Mungu kupandishwa kizimbani baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo walisema kuwa, kuna kila sababu ya viongozi wa juu kuangalia chanzo cha mmomonyoko huu wa maadili.

“Lazima kuna tatizo tu, haiwezekani kila siku viongozi tunaowaamini wanatuhumiwa kufanya matukio yanayokwenda kinyume na maadili, lakini bado wanakuwa hodari kwa totoz, kuna kila sababu ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa kufanya kila linalowezekana kuikabili hali hii kabla kizazi hakijaangamia,”alisema Josephine James wa Iringa mjini.

Naye Charles John wa Sinza jijini Dar es Salaam alisema kuwa, KKKT mara kwa mara limekuwa likikumbwa na kashfa mbaya hali inayowafanya watu wa pembeni kujenga picha tofauti.

Source: www.GlobalPublishers.info

No comments: