Monday, August 30, 2010

Wafu wanafufuka..!


Binti Amina Waziri, aliyefufuliwa huko yombo vituka na mmoja kati ya watenda kazi-Shepherd wa Nyumba ya Ufufuo na Uzima, siku ya jumanne tarehe 6 Julai 2010 majira ya saa kumi jioni.

Picha ya kwanza: Amina Waziri, binti aliyefufuka akiwa ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima. Picha ya pili; Bi. Halima, mama mzazi wa Amina Waziri akishuhudia jinsi binti yake alivyokufa na baadaye kufufuka!

Binti Amina Waziri(mwenye kanga za njano kulia) au kwa jina lingine Happy mkazi wa yombo vituka moja kati ya sehemu maarufu hapa jijini Dar aliyefufuka siku ya jumanne tarehe 6 Julai 2010. Anayefuata ni mama mzazi wa binti aliyefufuka, Bi. Halima ambaye aliamua kumpa Yesu maisha yake kwa muujiza mkuu wa kumfufua binti yake. Kushoto kabisa mwenye tai nyekundi ndio shepherd (mtenda kazi) wa nyumba ya ufufuo na uzima aliyeomba maombi ya kurudisha na hatimaye kumfufua binti Amina saa chache baada ya kukata roho. Mwenye suti ya kijivu ni Mpakwa mafuta wa BWANA, Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima. Wote wakimtukuza Yesu kwa Ufufuo na Uzima.

Source: http://ufufuonauzima.blogspot.com


4 comments:

Anonymous said...

Siku hizi za mwisho tutaona na kusikia mengi!!!

Anonymous said...

I just added your website on my blogroll. I may come back later on to check out updates. Excellent information!

Anonymous said...

I just added your website on my blogroll. Really enjoyed reading through. Excellent information!

Anonymous said...

Really great article with very interesting information. You might want to follow up to this topic!?! 2011