Saturday, December 4, 2010

Life Blessings at Faith Word Church

Faith Word Church.Ni moja kati ya makanisa yenye mafundisho mazuri sana (sound dcotrines) hapa nchini Tanzania.Likiwa chini ya mwangalizi mkuu wa makanisa hayo ulimwenguni Pastor Erastus Andrew,FWC lina matawi yake katika miji ya Dar es Salaam,Mkoa wa Pwani, Mwanza,Ukerewe na Pennsylvania nchini Marekani.Jijini Dar es Salaam FWC ipo eneo la mnazi mmoja kidongo chekundu karibu na jengo la ushirika,mkabala na stendi ya mabasi ya hekima na sumry yanayotokea mkoani Mbeya.
Ibada zao ni siku ya jumapili kuanzia saa 1-4 asubuhi, saa 5-7 mchana, saa 10-12 jioni (english service).Pia jumatano na ijumaa saa 11 jioni kila wiki. Pichani ni waimbaji wa Faith Word Choir chini ya mwalimu mahiri Sauti ya Nyika wakimtukuza Mungu katika moja ya ibada zenye umwagiko wa Roho Mtakatifu.
Waweza kuwafuatilia zaidi katika tovuti yao www.fwctz.org itakayokuwa hewani kuanzia mwenzi wa january mwakani.
Kwa mawasiliana zaidi waandikie info@fwctz.org

No comments: