Sunday, February 24, 2008

EAGT wafukuza wachungaji 32

Week hii kuna habari kuwa kanisa la Evengelist Assemblisies of God (EAGT) jimbo la kaskazini limewafukuza wachungaji wake 32 kwa kutotii maamuzi ya uongozi wa kanisa hilo ya kuwataka wachungaji wake wote kwenda Bible school wakasomee uchungaji.
Akizingumza kwa masikitiko makubwa mmoja wa wachungaji hao 32 waliofukuzwa kazi hiyo ya kulisha kondoo alisema kuwa anashangaa kuwa baada ya kulitumikia kanisa hilo kwa muda mrefu na kuisimamisha kazi ya Mungu kwa taabu na shida nyingi tangia kipindi cha migororo ya kanisa hilo na TAG, hivi sasa wao wanaonekana hawafai kumtumikia Mungu kwa sababu hawana elimu ya Bible school.
Kanisa la TAG(Tanzania Assembilies of God) lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu tangia mwanzoni mwa miaka ya 80 hadi 90 katikati.
Kuanzia kipindi hicho kanisa la EAGT limekuwa likiwatumia wachungaji ambao hawajaenda Bible school huku likionyesha mafanikio makubwa sana kwa kuwa miongoni mwa makanisa yanayokuwa kwa kasi sana.
Hata hivyo uongozi wa juu wa kanisa la EAGT nchini umekuwa ukiwataka wachungaji wake waote wasioenda Bible school wahakikishe wanapata elimu hiyo ya Biblia na kutoa taarifa kuwa wasiokubali uamuzi huo watalazimika wataondolewa kwenye nafasi zao za uchungaji.

6 comments:

Anonymous said...

kosa sio wachungaji ni misingi ambayo EAGT ilijiwekea tangu awali, pengine hawajui umuhimu wa shule, na pia hainiingii akilini kuwa kweli wamekaa chini na kujadili swala hili kwa upendo?? imeshindikana

Anonymous said...

tatizo la eagt ni kuwa hawajui jinsi ya kusuruhisha migogoro yao.kwao kufukuza wachungaji ni jambo la kawaida.

danny,

Houston

Anonymous said...

Hallow wapendwa hii siandiki ili mpablish, we dont have any christian blog more than this i dont know, kindly update this one everytime you can, congratulation you are doing well but, i like this blog to be efficient and attractive, i am in Canada you may use then to prepare some teachings or otherwise. please advice . hkalenga@mirarco.org

Maranatha said...

Shalom!
Sidhani kama tatizo ni Bible School (shule) japo kwa zama za leo shule katika huduma ni muhimu sana. Naweza kuamini kwamba si kwamba hawa wachungaji waliambiwa jana waende shule, la hasha bali walikuwa na muda wa kutosha kabisa (miaka) kujiandaa kwenda shule. Nachelea kusema kwamba haiyumkini walipuuzia kwa makusudi au kutingwa na majukumu. Kama walifanya makusudi kutokwenda shule huko ni kutokutii maagizo ya viongozi wako na wanastahili kukaa benchi. La kama ni kuna sababu ya msingi basi wapewe fursa nyingine waende wakasome sasa na sio wakati mwingine kuhubiri mahubiri yenye hadithi za uongo pasipo hata wao kujua wanadanganya.

Niweke mfano huu: Mhubiri mmoja akijawa na msisimko alinena kwamba Israel ni nchi kubwa yenye eneo kubwa kuliko hata Tanzania. Huyu mhubiri inaonesha kwamba hata elimu yake ya Jiografia ni hafifu. Sasa wapo wengi wa aina hiyo, hivyo ni muhimu waende wakanolewe ili kuepusha uongo usio wa kukusudia makanisani.

Mwanzoni ndio EAGT ilihitaji bora mchungaji kwa sababu ya uhaba uliokuepo na sio sasa. Ni kama vile enzi za walimu wa UPE shule zilihitaji waalimu lakini leo hii hakuna kazi ya ualimu mpaka uwe na cheti. Naomba nikubaliane na huo uongozi kwa kuwapa hiyo changamoto hao wachungaji waende shule. Manabii wote na watumishi wakubwa tusomao ktk biblia waliketi chini wakafundishwa, SHULE!!!!

Anonymous said...

Wao mtumishi Chalu, umenena vizuri mimi nimekuwa mu-EAGT for 6 years sasa na nimekuwa TAG- for 4 years, umesema na umenena kweli.Na ninafahamu vyema katiba za haya makanisa mawili.wakati TAG huwa wanajitahidi hata kuwalea wachungaji wao kwa fedha zitokazo jimboni hali ni taoafuti sana EAGT.EAGT unakula kadiri ulivyo na wingi wa kondoo.MAKANISA MENGI MAPYA YANAYOANZISHWA CHANZO NI EAGT!!..sasa je hawa wachungaji wataishi vipi na wao wamezoea fungu la kumi?? si ndio mwanzo wa kuanzisha makanisa yao?? .wengi hawana kazi, wamelelewa hivyo.sijafurahi kufukuzwa kwa o wala sijakasirika bado nawazua mengi hapa.mstakabali wa kanisa hili na hasa mzee yule akiondoka(siombei hivyo)!!.Kuna mchangiaji amesema huwa hatuna karama ya kusuluhisha matatizo yetu.Nakubali

Kalenge

Anonymous said...

Mtumishi Kalenge,
Umeongelea kitu muhimu sana.Japo hatuombei hivyo lakini tunaishi duniani na lazima sasa kanisa lijiandae mrithi au warithi baada ya mzee yule kuondoka(Mungu apitishiliye mbali)
Nakumbuka miaka ile ya 80 na 90 moto ulikuwa unawaka sana kwenye mikutano ya mzee.
Lazima kanisa lifike mahali liwe na plan na liache kufukuza watu ovyo.
Mwanasayuni,

Tabora,Tanzania