Wednesday, February 27, 2008

ILIWEZEKANAJE YONA KUKAA TUMBONI MWA SAMAKI KWA SIKU TATU?


Yawezekana kabisa ukawa una maswali mengi juu ya uwezekano kwamba Yona yule aliyetumwa kuhubiri Ninawi aliweza wezaje kukaa ndani ya tumbo la samaki pasipo kumeng’enywa kama vyakula vingine kwa siku tatu? Wanasayansi wanajaribu kufafanua namna ambavyo jambo hilo linawezekana na hivyo kuthibitisha kwamba Mungu wetu yu hai na anaweza kufanya mambo makubwa na ya ajabu.

Ukiaacha ya Yona zipo hadithi nyingi za watu waliomezwa na nyangumi na kisha kutoka wakiwa hai. Hizi sio hadithi za yule nondo mla watu wa ziwa Jipe bali ni kweli. Samaki mkubwa aitwaye "Sea Dog" (Carcharodon carcharias), anayepatikana kwenye maji ya bahari yenye mkondo joto huweza fikia urefu wa futi 40. Kunako miaka ya 1758 mvuvi mmoja bahari ya Mediterania aliwahi kuangukia baharini na kumezwa na samaki wa aina hii. Nahodha wa meli hiyo aliamuru bomu lipigwe kumlenga yule samaki. Matokeo yake ni kwamba yule samaki alimtapika mvuvi akiwa hai pasipo madhara yeyote. Maka 1891, James Bartley- mvuvi mwingine nae alimezwa na nyangumi katika visiwa vya Falkland na alikaa ndani ya nyangumi huyo kwa zaidi ya masaa 48 mpaka samaki huyo alipovuliwa na kupasuliwa. Ilimchukua wiki mbili kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida lakini alipona. Wako watu wengi tu ambao wanatajwa kumezwa na kisha kutapikwa na nyangumi wakiwa hai.

Wataalamu wa mambo ya kale wanaandika kwamba Babeli ilikuwa na utamaduni wa kuamini Samaki Mtu (Nguva). Wanasema kunako mwanzoni mwa ustaarabu (civilization) Ukaldayo na Babeli uliamini sana maongozi ya mtu ambaye alikuwa nusu mtu nusu samaki aliyetoka majini. Katika siku za Yona, Ninawi nayo pia ilikuwa katika mfumo huo wa kiimani na waliamini katika roho iliyoleta ujumbe kupitia mtu aliyetokea/kuibuka kutoka majini/baharini kama nusu mtu, nusu samaki. Kwa maana hiyo basi hatushangai kuona hata ujumbe wa Yona ulipata kukubaliwa kwa haraka sana na watu wa Ninawi hata kutubu na kuziacha dhambi zao, na pia twasoma katika biblia kwamba Mungu aliusamehe mji wa Ninawi.

Tunaposoma leo katika biblia juu ya habari za Ninawi ni kama hadithi lakini ni mji uliokuwapo na wanasayani wanathibisha masalia yake kama yalivyochimbuliwa huko Babeli yajulikanayo kama "Neby Yunas," . Katika masalia hayo kuna kumbukumbu za jina la YONA (Yunas) jambo linalothibitisha hadithi hiyo ya Yona na pia waliweza kugundua masalia yaliyoharibika ya kasri ya mfalme wa Ninawi.

Imefasiriwa na kufupishwa na:
Chalukulu John Bilinzozi – Oslo
E-mail: chalu.john@gmail.com
(This is not official translated version, the english version remains authentic) -
http://www.grmi.org/renewal/Richard_Riss/evidences/8jonah.html

Kwa ufahamu zaidi juu ya habari za Yona soma kitabu cha Yona katika biblia – Agano la Kale.

1 comment:

Anonymous said...

Nilikuwa sina habari kama kuna watu washawahi kumezwa na samaki na wakatoka wakiwa hai.
hii ni habari mpya kwangu, hata hivyo Mungu ni Mungu wa yote , yale yanayowezekana na yale yasiyowezekana.
Thank Mtume for this useful post..

Ubarikiwe

Baba Chinyemi